Kigogo Chadema kizimbani kwa tuhuma za ugoni

Kigogo Chadema kizimbani kwa tuhuma za ugoni

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Chadema(77).jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Rorya, mkoani Mara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tai, Masirori Kyorang, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Shirati, akikabiliwa na kesi ya kushikwa ugoni na mke wa mlinzi wa Mbunge wa Jimbo la Rorya.

Akisoma hati ya mashitaka hayo mahakamani hapo mbele ya Hakimu, Dock Nyatega, Mwendesha Mashitaka wa Polisi alidai kuwa, Masirori alikamatwa Julai 24 kwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ya Tripo Kabwana akiwa na mwanamke huyo Pendo Omolo.
Alidai kuwa, mume wa mwanamke huyo ambaye ni mmoja ya walinzi wa Mbunge wa Jimbo la Rorya katika majengo yake wilayani humo, Ochieng Ninja alipata taarifa ya kuonekana mke wake ndani ya nyumba ya kulala wageni akiwa na Mwenyekiti huyo wa Chadema Wilaya ya Rorya.

Alieleza kuwa, mlinzi huyo baada yakufika katika nyumba hiyo ya wageni aliomba msaada wa watu ambao walijitokeza na kuwakamata mtuhumiwa na mwanamke huyo. Masirori alikana mashitaka dhidi yake na amepewa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Julai 29, mwaka huu. Umati mkubwa wa watu ulijitokeza mahakamani hapo iliza kesi hiyo ya kukamatwa ugoni.

CHANZO: NIPASHE
 
Sasa tuchange nini kama kesi iko mahakamani?!
Asante kwa taarifa anyway!
 
Ni baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa wananchi, kweli chadema ni hatari!
 
Baada ya kiongozi mmoja mwandamizi wa chadema kuhusishwa na uporaji wa mke wa mtu, kashfa hii inaendelea kuitafuna safu ya viongozi wao huku kiongozi mwingine kutiwa korokoroni kwa kupora mke wa mtu! habari kamili gazeti la nipashe---Home

Jee, chadema wataendelea kufumbia macho kashfa hizi mpaka lini? jee, chadema wanaiga staili ya CCM ya kulindana?
 
Hiyo itakuwa mbinu ya maccm anyway kila mtu ana udhaifu wake hata bosi wa pale nyumba kuu ana mtoto kila wilaya.
 
Baada ya kiongozi mmoja mwandamizi wa chadema kuhusishwa na uporaji wa mke wa mtu, kashfa hii inaendelea kuitafuna safu ya viongozi wao huku kiongozi mwingine kutiwa korokoroni kwa kupora mke wa mtu! habari kamili gazeti la nipashe---Home

Jee, chadema wataendelea kufumbia macho kashfa hizi mpaka lini? jee, chadema wanaiga staili ya CCM ya kulindana?

we ni mpuuzi kwani hilo swala ni la cdm au la huyo muhusika kwani cdm imepelekwa mahakamani?....au hiyo dushelele alioitumia jamaa ni ya chama.....
 
Huyu yafaa amfuate chemba ccm!Duu wanaume mabosi tumezidi kuwala wake wa wafanyakazi wetu hili limekua ni tatizo sugu
 
Huyo alikamatwa ugoni na mke wa mbunge waandishi wakabadili na kusema ni mke wa mlinzi wa mbunge.
 
we ni mpuuzi kwani hilo swala ni la cdm au la huyo muhusika kwani cdm imepelekwa mahakamani?....au hiyo dushelele alioitumia jamaa ni ya chama.....

Matusi si dawa! ila Chadema ni muhimu wajitenge na kashfa za ngono kama wanataka kuungwa mkono na wananchi wenye maadili!
 
Yeah, ila nimesikitika! Sana, ila c ajabu ni njama ya wanaflaniflani hivi!
 
Mmeishiwa mnaacha kujadili Tanzania ilivyokwamishwa kimaendeleo na KIJANI, mnajadili maisha binafsi ya mtu! Wewe umeathirika wapi!
 
Si mlaumu kafuata mkondo wa viongozi wake wa chama taifa kwani yeyesiyo binadamu?
 
we ni mpuuzi kwani hilo swala ni la cdm au la huyo muhusika kwani cdm imepelekwa mahakamani?....au hiyo dushelele alioitumia jamaa ni ya chama.....
Maswari yako yote uliyouliza majibu yake yote ni ndiyo.
 
Back
Top Bottom