Kigogo aumbuliwa mbele ya pinda

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Mkazi wa Igunga, Abel Mkinga, amefichua uozo wa rushwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ukimhusu Ofisa wa Halmashauri ya wilaya hiyo...

Ofisa huyo (hakumtaja jina), amedaiwa kuomba rushwa ya Sh 600,000, ili atoe kibali cha kufanya biashara kwa raia huyo.

Hata hivyo, Pinda alimuita Mkinga na kumtaka Mkinga amtaje ofisa huyo hadharani, lakini alikataa kwa kulinda usalama wake, kisha aliandika jina lake (ofisa) kwenye karatasi na kumkabidhi.

Hatua ya Mkinga ilifikiwa juzi wakati Pinda, alipokaribisha maswali, maoni na maelezo yanayohusu masuala mbalimbali, zikiwemo kero zinazowakabili wakazi wa Igunga. Pinda alitoa fursa hiyo baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sokoine wilayani humo.

Kwa mujibu wa Pinda, wananchi hao walipaswa kuuliza masuala yaliyo nje na sekta za umeme, daraja na barabara, ambavyo ujumbe wake ulishapata maelezo rasmi. Mkinga akiwa mtu wa pili kuzungumza, alisema alijenga banda la biashara, na alipofuatilia kibali katika halmashauri hiyo, alitakiwa kutoa rushwa lakini alikataa.

"Kwa vile nilikataa kutoa hiyo rushwa, hadi leo hii hilo banda halijaisha, sijaweza kufanya chochote," alisema kwa sauti ya uchungu. Alisema, alifuatilia haki yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimara, ambapo alielekezwa kwa maofisa wa ngazi ya chini katika halmashauri (hakuwataja) ambao hata hivyo alijibiwa kwamba kwa kuwa (Mkinga) ni mwanasiasa, hawawezi kumsikiliza.

Mkinga alisema watumishi wa halmashauri hiyo wamekithiri kwa ubabe na kwamba hawana nafasi ya kufanya majadiliano pindi inapotokea migogoro baina yao na wananchi. Akizungumza katika mkutano huo, Pinda aliahidi kuifanyia kazi kero hiyo na kumtaka Kimario, afuatilie na kutoa jawabu ifikapo Jumamosi ijayo, atapofanya majumuisho ya ziara yake.

Pia, Pinda aliwataka wakazi hao wasikatae kutoa rushwa wanapoombwa na maafisa kama hao, lakini wafikie hatua hiyo baada ya kuwasiliana na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom