benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,192
"IMEANDIKWA KWENYE GAZETI RAIA MWEMA"
Gwiji wa mazingira na uhifadhi nchini Gerald Bigurube amempongeza Naibu Waziri mstaafu, mbunge wa zamani wa Ngorongoro, Saning' o ole Telele kuamua kwa hiyari kuhamia Msomera, Handeni, Tanga.
Telele aliyekuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne, alijiandikisha rasmi kuhamia kijiji cha Msomera, kupisha uhifadhi katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Bigurube aliyehudumu serikalini miaka zaidi ya 40 na mashirika ya uhifadhi kitaifa na ya kimataita, aliliambia gazeti RAIA MWEMA juzi, kuwa uamuzi aliochukua kiongozi huyo ni mzuri na umekuja wakati mwafaka.
"Siku zote kiongozi wajibu wake ni kuonesha njia, hivyo uamuzi aliochukua ametambua uamuzi wa Serikali ni uamuzi muhimu kwa maslahi mapana ya Taifa.….nampongeza sana Telele," alisema Bigurube ambaye pia alihudumu kama Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Bigurube baada ya kutaafu serikalini, pia alihudumu kama Meneja Miradi wa Shirika la Uhifadhi la Frankfurt Zoological Society Tanzania.
Mwaka 2018 alitunukiwa tuzo maalumu ya Ujerumani kwa Afrika kama mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania akiwa na mwenzake, Clovis Razafimalala wa Madagascar.
Bigurube alisema ni wakati sasa wa jamii kujua kadri Ngorongoro inavyostawi, Taifa linanufaika na uwezo wake, kwa hiyo chochote kinaweza kufanyika ili azma ya Serikali kufikiwa ni vema kutekelezwa kwa mustakabali mzuri wa Taifa.
Telele alisema aliamua hivyo kwa sababu ya haiba na wadhifa wake alipokuwa serikalini. Alisema kama kiongozi aliyeitumilia Serikali muda mrefu, asiwe moja ya vikwazo kwa wengine kuchukua uamuzi huo kutokana na hadhi aliyokuwa nayo serikalini na jamii kwa ujumla.
"Najua mambo haya baadaye yatasemwa mengi, watasema huyo mzee tulikuwa tunamtegemea ni kama ametutelekeza, ametuacha na hivi hatuna pa kushika sasa. "Ingawa ni vigumu sana mtu, kuhama eneo alilozaliwa, aliloishi kwa muda mrefu mpaka anastaafu akiwa pale, tena anazeekea pale, ni ngumu sana kufanya uamuzi," alisema Telele.
Watu wafanye uamuzi kwa sababu maisha ni mwamuzi.….muda si mrefu, hifadhi hii inaweza kupotea kutokana ongezeko la watu, mifugo na mengine," alisisitiza.