Kigogo aliyefukuzwa ATCL ajibu mapigo

Kigogo aliyefukuzwa ATCL ajibu mapigo

sasa unazingua, si umesema jina lipo kwenye story...

Mkuu unataka utafuniwe kila kitu? Kitendo cha kusema jina tunalo halafu katika hiyo story wanamtaja aliyefukuzwa ni wazi washa reveal hilo jina,kama upo interested kujua jina just google cashier aliyefukuzwa ATCL utalipata.
 
Serikali ingewekeza zaidi katika kuboresha airports badala ya kuzidi kupoteza pesa kuifufua ATC. Serikali iruhusu makampuni kushindana katika biashara ya usafiri wa anga huku ikikusanya kodi ndio biashara ya ukweli kwa serikali yetu. Tukiendelea kushindana kwa vile Burundi au Kenya wana ndege zao tutaendelea kuzika pesa. Mbona Marekani haina shirika la ndege linalomikiwa na serikali lakini kuna mashirika mengi ambayo yanatoa huduma kwa ushindani?
 
Ndiyo umeamua kumwaga ugali baada ya kumwagiwa mboga, ngoja vyombo vya usalama vianze kuwatoa upepo na wao wapate mgao kufunika/kuficha huo WIZI wenu ili msipelekwe mahakamani,huna hata aibu kujitangaza hadharani wewe ni MWIZI.
 
KIGOGO mmoja aliyekuwa na dhamana kubwa katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), jina tunalo, ameweka mambo hadharani kwa kusema kuwa ametolewa kafara kwa kufukuzwa na kutuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za shirika hilo zinazokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani 55,000.

Kigogo huyo alikiambia chanzo chetu jana jijini Dar es Salaam kuwa katika ubadhirifu huo hakuwa peke yake bali alishirikiana na vigogo wenzake wawili ambao mwisho wa siku wamemgeuzia kibao yeye.

Akizungumza kuhusiana na sakata hilo, kigogo huyo alibainisha kuwa alishirikiana na kigogo wa Uhandisi, na wa Rasilimali Watu.

"Mara ya kwanza Novemba 19, yule wa uhandisi alichukua dola 12,100 za mgawo kisha Januari 19 mwaka huu, akachukua tena 2,700 ambazo alisema ni za matibabu ya mwanae aliyepo Urusi baada ya kupata ajali mbaya nchini Ukraine na yule wa rasilimali watu Desemba 22 mwaka jana, alichukua dola 9650, kwajili ya mambo ya kifamilia na ujenzi wa dharura"

"Tulikubaliana kuwa tutaificha menejiment kuhusu uchotaji huo wa fedha na kisha wao wawashe moto kwa kuishtaki kampuni hiyo ya Kenya kwa kukiuka mkataba na kuidhalilisha kampuni yetu, pia hatukukubaliana kuwafukuza wafanyakazi wa chini lakini wamekiuka kwa kumfukuza cashia pasipo hatia" alisema kigogo huyo.

Aidha kigogo huyo alieleza kuwa washirika wake hao kwa pamoja walimgeuka na kumfanya yeye mbuzi wa kafara ilhali wanaufahamu ukweli wa mambo kuwa wote walihusika na walijua kinachotokea wakati wakiidhinisha wa fedha taslim.

"Wamenigeuka. Naomba na wao wachukuliwe hatua stahiki kama ile iliyochukuliwa dhidi yangu bila kupepesa macho. Wao ndiyo walioidhinisha ulipwaji wa pesa hizo ila leo wamenigeuka,"

"Kila kitu wanakifahamu na wao ndiyo waliahidi kuwa watashughulika na kuishawishi menejiment kufungua kesi za madai na fidia. Pia kama haitoshi wakaenda kuiambia bodi kuwa mimi ndiye niliewarubuni. Mungu atawalipa sawa na waliyonitenda mimi " alibainisha kigogo huyo.

Alisema kuwa fedha hizo ni sehemu ya malipo ya ndege waliyoikodisha toka Kenya, ambayo kila mmoja wao alikuwa akitambua kuwa malipo yote hufanyika kwa njia ya hundi na sio kwa fedha taslim.

Pia kigogo huyo alidai kuwa lengo lao lilikuwa kutaka kuishtaki kampuni hiyo, ambayo kesi hiyo ingechukua muda mrefu na hata uchotwaji wa fedha hizo usingejulikana.

"Kulikuwa na mkakati wa kuwasha moto mkubwa kwa kuishtaki kampuni hiyo ya Kenya na kuendesha kesi ambayo ingechukua muda mrefu kujua kama kulikuwa na uchotaji wa fedha hizo, maana katika mzozo huo ambao tungeanzisha kila mmoja wetu angetoa madai yake, hivyo isingekuwa rahisis kujua ni nani anambambikizia mwenzake lakini baada ya kubainika wenzangu wameruka kwenye kikao cha Bodi, hivyo nina amini mungu atanilipia tu" alidai kigogo huyo.

Alisema anashangaa kuona watu wamemgeuzia kibao na kuamua kutoa kwenye vyombo vya habari huku wakijua ukweli wa jambo hilo.

Lione linaongea kama kuku mtamu.....!
 
kaamua kuwangeleja wenzake ?.

kwa nini hawa watu, hawapelekwi mahakamani kwa wizi ?.

alafu JK yeye anacheka cheka tu.

Yule albino angemtoa utumbo, si uliona mateke yake, unacheka cheka tu
 
Kwa kweli sijui wapi inaelekea nchi yetu!
Huyu mtu aliyejitapa mbele ya umma na kuomba Mungu atamlipia kwa wizi wao hawajakamatwa tuu yeye na wezi wenzake? it's unbelievable!
 
Sawa CCM ndo was kulaumiwa mpaka hapo
 
Back
Top Bottom