Kigogo afanyiwa umafia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo afanyiwa umafia

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Mar 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Amani [​IMG]
  [​IMG]

  Na waandishi Wetu
  Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Jafari a.k.a Osama au Kigogo, mkazi wa Mtaa wa Itungi uliopo Magomeni Mwembechai, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alijikuta akipatwa na aibu ya mwaka baada ya kufanyiwa umafia wa kutisha, chanzo kikidaiwa kuwa ni kukutwa na mke wa mtu... Kigogo afanyiwa umafia

  Amani [​IMG] [​IMG]
  Tukio hilo la aina yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika nyumba ya kulala wageni (jina tunaliminya) iliyopo Manzese Tip Top kufuatia madai ya Kigogo huyo kukutwa na mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina moja la Joha ambaye ni mke wa jamaa mmoja aliyefahamika pia kwa jina la Jafari.

  Akilimwagia udaku Amani juu ya tukio hilo, mtoa habari wetu aliyeomba chonde chonde jina lake lisichorwe gazetini alidai kwamba, awali alisikia vurumai kutoka ndani ya moja ya chumba cha gesti hiyo na kufanikiwa kupenya ndani.
  Akadai kwamba, alipofika kwenye ‘korido’ aligundua kuwa kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba hicho ni madai ya kuchukuliana mwanamke licha ya kwamba hakukuwepo na ushahidi wa kuthibitisha hilo.

  Mtoa habari huyo aliendelea kudai kuwa, kufuatia tafrani hiyo iliyochukua takribani dakika 7, alifanikiwa kuingia ndani na kufotoa picha kadhaa (zinazoonekana ukurasa wa mbele), kisha kuondoka katika eneo hilo bila kujua kilichoendelea baadaye.

  Baada ya picha na maelezo ya tukio hilo kutua katika dawati la Amani, timu ya Waandishi Wetu ilifanya jitihada za kumtafuta Osama ambapo ilifika katika eneo analoishi, Mtaa wa Itungi Mwembechai Magomeni, jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kumtia machoni kigogo huyo.

  Hata hivyo, baada ya Waandishi Wetu kupaki gari pembeni na kushuka ili kumfuata ‘mkubwa’ huyo kwa lengo la kumhoji juu ya kilichotokea, ghafla alitoweka eneo hilo na hata walipojaribu kuwauliza watu waliokuwa karibu naye, walidai kutomfahamu.

  [​IMG]
  Jitihada za kumsaka jamaa huyo hazikuishia hapo kwani ‘polisi’ wa Amani walifika hadi katika nyumba anayodaiwa kuishi Osama, lakini pia walikosa ushirikiano kutoka kwa majirani ambao nao walionekana kujua kilichotokea ila waliamua kumfichia aibu kwa kueleza kuwa, hawamjui na wala hawajui chochote.

  Aidha, safari ya ‘makachero’ hao ilianza kuelekea kwa mjumbe wa mtaa huo aliyetajwa kwa jina moja la Saidi, lakini nako jitihada za kupata ‘data’ za kigogo huyo ziligonga mwamba baada ya kiongozi huyo kudaiwa kuwa katika mihangaiko yake kwa wakati huo.

  Timu ya Mapaparazi Wetu juzi majira ya saa 10:00 jioni, ilifika katika gesti inayodaiwa kutokea tukio hilo na kufanikiwa kuongea na mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya wageni aliyejitambulisha kwa jina la Protas Daudi, lakini katika hali ya kushangaza alikataa kata kata ishu hiyo kutokea katika eneo hilo.

  “Kaka hapa kwanza hatupangishi watu wa ‘short time’ na kama mnadai tukio hilo lilitokea hapa, sisi hatuna taarifa yoyote ila tunaomba chonde chonde msije mkaitaja gesti yetu katika habari yenu, mtatuharibia biashara,” alisema Daudi.

  Gazeti hili linaendelea kuchimbua undani wa sakata hilo na mara baada ya kukamilisha ‘data’ litawaletea upande wa pili wa habari hii.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,349
  Likes Received: 22,195
  Trophy Points: 280
  Umbea mtupu na uzandiki.
  Habari haina kichwa wala miguu
   
Loading...