Kigoda cha mwenge wa uhuru chaibiwa jijini Arusha


kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
32,016
Likes
5,334
Points
280
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
32,016 5,334 280
[h=3]KIGODA CHA MWENGE WA UHURU CHAIBIWA JIJINI ARUSHA....[/h]KATIKA hali isiyo ya kawaida na inayoashiria uzembe katika ulinzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, juzi kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips katika Kata ya Sekei jijini Arusha, Hamad Rashid (32) aliiba kiti (kigoda) cha kukalishia Mwenge.
Kuibwa kwa kiti hicho kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas. Kiti hicho hutumika kuwekea Mwenge wa Uhuru unapokuwa katika mbio zake nchi mzima.
Tukio la kuibwa na kisha kukamatwa kwa mtuhumiwa lilitokea juzi saa 11 jioni Sanawari eneo la Mataa. Eneo hilo ndilo lilipangwa kwa ajili ya mkesha wa Mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Arusha.Kufuatia tukio hilo, Kamanda Sabas aliyetafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia tukio hilo, alikiri kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo alishakamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda Mwenge pamoja na kiti hicho.Alisema tukio hilo lilitokea wakati Mwenge huo pamoja na wakimbizaji wake kitaifa, kimkoa na viongozi wengine wakiwa katika harakati za kusoma salamu za utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya ratiba ya utangazaji wa ratiba ya mkesha kutolewa.Alisema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, alionekana kwa muda mrefu akiwa amesogelea gari lililokuwa limebeba kiti hicho kilichoelezwa na kamanda kuwa kilikuwa cha akiba.


Alisema mara baada ya wizi kijana huyo alikamatwa na katika mahojiano alisema alikuwa anataka kukiangalia tu na kwamba haikuwa nia yake kukiiba na kuomba msamaha.Hata hivyo alisema polisi wanaendelea kumhoji ili kubaini dhamira halisi ya kukichukua kiti hicho.Alisema mara baada ya upelelezi wa kesi hiyo, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yanayomkabili ya wizi wa kiti hicho cha Mwenge wa Uhuru.


Mwenge huo wa Uhuru uliingia Arusha Juni 3 mwaka huu ukitokea mkoani Manyara na utakimbizwa katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Arusha kabla ya kukabidhiwa kwa mkoa wa Mara Juni 11, yaani Jumanne ijayo.
 
Mshomba

Mshomba

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Messages
1,629
Likes
207
Points
160
Mshomba

Mshomba

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2013
1,629 207 160
Kweli waTz hamnazo
 
Ndallo

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
7,390
Likes
1,568
Points
280
Ndallo

Ndallo

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
7,390 1,568 280
Nakumbuka kauli ya muheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema wakati ule wa kiny'anyiro cha kugombea uraisi kwa tiketi ya NCCR MAGEUZI kuhusu Mwenge huu, alidai akichukua nchi atapiga marufuku mbio za mwenge kwakua zimepitwa na wakati!

Tukija kwa mgombea aliyegombea uraisi kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na alisema akichukua nchi atauweka mwenge huu katika nyumba ya makumbusho!

Tafakari watu wameiba kiti cha kuuwekaa mwenge leo! Kesho kutwa tusishangae tukasikia mwenge umeibiwa!

My Take nahisi watu wameshachoka na hii kitu inaitwa Mwenge wa Uhuru!
 
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
21,523
Likes
18,140
Points
280
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
21,523 18,140 280
Huyo jamaa bora angeiba mwenge wenyewe.!!!!

Tumechoka na uzinzi wa mwenge.!!
 
Captain22

Captain22

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Messages
629
Likes
78
Points
45
Captain22

Captain22

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2011
629 78 45
Katika mkesha wa mwenge jiji la Arusha pale sanawari, kidoga cha kuwekea mwenge kiliibiwa.
 
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,994
Likes
496
Points
180
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,994 496 180
Wacha kiibwe!
Ingependeza na mwenge ukaibwa manake ni upunguani mkubwa kukimbiza moto eti unatumia mabilioni kufungua miradi ya milioni
 
S

Schofild

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Messages
204
Likes
5
Points
35
S

Schofild

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2011
204 5 35
Mi nautaka huo mwenge nichomoke nao.
 
M

majid musisi

Senior Member
Joined
Apr 14, 2013
Messages
185
Likes
1
Points
0
M

majid musisi

Senior Member
Joined Apr 14, 2013
185 1 0
Hicho kigoda kinafaa kuwekwa counter kwenye bar!!
 
N

NOKIA100

Member
Joined
Apr 17, 2013
Messages
31
Likes
0
Points
0
N

NOKIA100

Member
Joined Apr 17, 2013
31 0 0
aah! kigoda tu? wangechukua na hicho kibatari kwani ni usumbufu kwa watumishi na hasa polisi
 
CYBERTEQ

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Messages
7,415
Likes
264
Points
0
CYBERTEQ

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2012
7,415 264 0
KIGODA CHA MWENGE WA UHURU CHAIBIWA JIJINI ARUSHA....

.
Sasa hao askari waliozunguka huo moto wanaota moto ama? Huyo mwizi alikuwa anachukua chake mapema, watu wanaiba tembo na twiga hamsemi, ije kuwa jamaa amechukua stuli ya kwenda kukalia nyumbani kwake!
 

Forum statistics

Threads 1,272,943
Members 490,211
Posts 30,465,430