Kigezo cha UNESCO World Heritage hakitoshi kuwaondoa Wamaasai Ngorongoro

Kigezo cha UNESCO World Heritage hakitoshi kuwaondoa Wamaasai Ngorongoro

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Kwa miaka ya karibuni, mjadala kuhusu hatma ya jamii ya Wamaasai ndani ya Ngorongoro Conservation Area umeendelea kuchukua sura mpya. Kauli ya Samia Suluhu Hassan kwamba Ngorongoro ni moja ya maeneo machache sana duniani yaliyo ya kipekee ndani ya UNESCO World Heritage Sites imezua mjadala mkali.
images - 2026-03-12T195556.355.jpeg

Wapo wanaoona kauli hiyo kama njia ya kuhalalisha sera za kuondoa jamii za asili ndani ya eneo hilo kwa kisingizio cha uhifadhi wa urithi wa dunia.

Hakuna ubishi kwamba Ngorongoro Conservation Area ni hazina ya kipekee kwa Tanzania na dunia ila tusijiachie kupita maelezo kama Chaneli ya Safari TV, dunia ina hazina kibao bora. Mandhari yake, wanyamapori wake, na historia ya binadamu katika eneo hilo vinaifanya kuwa sehemu muhimu sana ya urithi wa dunia uliotambuliwa na UNESCO.
images - 2026-03-12T200206.336.jpeg

Hata hivyo, hoja inayojitokeza ni kama hadhi hiyo ya kimataifa inaweza kuwa sababu ya kuwatenga au kuwaondoa watu waliokaa hapo kwa karne nyingi.
images - 2026-03-12T200224.875.jpeg

Kwa mtazamo wa kitaaluma, watafiti wengi wameonya dhidi ya sera za uhifadhi zinazotenganisha binadamu na mazingira yao ya jadi. Mwanahistoria wa mazingira Mark Dowie katika kitabu chake Conservation Refugees anaeleza kuwa katika sehemu nyingi duniani, miradi ya uhifadhi imewageuza watu wa asili kuwa “wakimbizi wa uhifadhi.”
images - 2026-03-12T200351.060.jpeg

Anabainisha kuwa jamii ambazo kwa muda mrefu zimeishi sambamba na mazingira mara nyingi ndizo zinazolinda bioanuai kwa njia endelevu zaidi kuliko mifumo ya uhifadhi inayowaondoa kabisa.
images - 2026-03-12T200049.067.jpeg

Hakuna watu wanaojua mazingira na ecosystem ya Ngorongoro kuwazidi Wamaasai, sio Msukuma wala Mpemba wala Mhehe. Wamaasai wao ndio walinzi wa Ngorongoro. Hoja hii inaungwa mkono pia na mwananthropolojia John M. MacKenzie ambaye katika kazi zake kuhusu historia ya hifadhi za taifa anaonyesha kuwa mifumo mingi ya uhifadhi ilianzishwa wakati wa ukoloni, mara nyingi bila kuzingatia haki za jamii za wenyeji.
images - 2026-03-12T200013.846.jpeg

Ndani ya bara la Amerika, mfano mzuri ni hifadhi ya taifa ya Yellowstone National Park inaonesha mabadiliko ya mtazamo. Ingawa katika karne ya 19 jamii za wenyeji ziliondolewa.
images - 2026-03-12T195943.815.jpeg

Leo serikali na watafiti wanajadili namna ya kurudisha ushiriki wa makabila ya asili katika usimamizi wa hifadhi hiyo. Vilevile katika Grand Canyon National Park, baadhi ya jamii za kiasili bado zina uhusiano wa kitamaduni na kiroho na eneo hilo.
images - 2026-03-12T195720.095.jpeg

Barani Asia pia katika hifadhi ya Sagarmatha National Park – nyumbani kwa Mlima Everest – jamii ya watu wa Sherpa imeendelea kuishi ndani ya hifadhi hiyo huku ikishiriki katika shughuli za utalii na uhifadhi. Hii inaonyesha kuwa uwepo wa watu wa asili haupingani moja kwa moja na ulinzi wa mazingira.
Maasai-Tribe-1.jpg

Barani Ulaya pia kuna mifano ya jamii zinazoishi ndani au karibu na maeneo ya hifadhi. Katika hifadhi ya Lake District National Park, wakazi wa eneo hilo wameendelea kuishi na kufanya shughuli za kilimo na utalii huku wakihifadhi mazingira ya kihistoria na asili.
images - 2026-03-12T195640.153.jpeg

Kwa mtazamo huu wa kimataifa, swali muhimu linabaki: je, uhifadhi bora ni ule unaowaondoa watu au ule unaowashirikisha? Tafiti nyingi za kisasa zinaelekea kuonyesha kwamba ushiriki wa jamii za wenyeji unaweza kuwa nguzo muhimu ya uhifadhi endelevu.
images - 2026-03-12T195629.466.jpeg

Acheni kutumia majukwaa kuonesha kuwa Ngorongoro ni salama bila Wamaasai wakati mnauza maeneo ili mahoteli makubwa yasimame ni UJINGA.
images - 2026-03-12T195556.355.jpeg

Ngorongoro si tu mandhari ya kuvutia bali pia ni nyumbani kwa ndugu zetu Wamaasai kwa kigezo cha historia, utamaduni na maisha yao. Kwa hiyo, mjadala kuhusu mustakabali wa eneo hilo haupaswi kuwa tu wa kisiasa au kiuchumi, bali pia wa kimaadili na kitaaluma. Tafuteni muda mkae na wazee wa kimila mjifunze historia na utamaduni wa Wamaasai.
images - 2026-03-12T200436.252.jpeg

Najiuliza swali dogo sana, Zanzibar kuna eneo la Stone Town, kwanini asiwaambie wazanzibar waondoke hapo ili kulinda mazingira, tukumbuke kuwa Stone Town nayo ni UNESCO World Heritage Site. Au ndio double standard kama kawaida?
 
Awafukuze stone town unataka wampige albadili ya rovu la shingo...
Sio muda utamsikia waziri mwenye sekta hiyo atasema "msipohama kwa hiari basi mtahama kwa viboko"

Serengeti pale kuna ndugu zetu walimu,manesi,watendaji wanapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa kama wale wauza urojo wa stone town.
 
Kuwa mgeni kwenye niliyozaliwa huwa haipo.
Any violence plus me you're gone.
 
Awafukuze stone town unataka wampige albadili ya rovu la shingo...
Sio muda utamsikia waziri mwenye sekta hiyo atasema "msipohama kwa hiari basi mtahama kwa viboko"

Serengeti pale kuna ndugu zetu walimu,manesi,watendaji wanapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa kama wale wauza urojo wa stone town.
albadili ya rovu la shingo 😃
 
Back
Top Bottom