Kigezo cha dini katika mapenzi

mezamate

Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
40
Reaction score
10
Aisee mimi bwana nina mpenzi wangu ambaye tunampango inshaallah miaka miwili ijayo tuoane.

Sasa nimejaribu kuleta hili swala kwa wazazi wangu japo sikuwa rasmi lakini wanaonekana kama hawajapenda na mipango yangu ya kuoa msichana mkatoliki wakati mimi ni sabato.

Msichana wangu hana tatizo juu kubadili dini lakini hata hivyo bado wazazi kama wanataka msabato pure.

Isitoshe huyo msabato sijampata bado ila huyu binti namjua vizuri mpaka wazazi wake.

Napata wakati mgumu na hili swala kwamba niwafurahishe wazazi au nafasi yangu?
 
acha nimeze mate kwanza! ila kaka kua makini na moyo wako! Kwanza je imani yako inakuambiaje juu ya hilo? je kwanin ww usiwe mkatoliki?
 
Mkuu fanya maamuzi mapema kabla huyo binti hajaumia...

washawishi wazazi wako wakubaliane na wewe kwanza nafuu wote ni wakirstu.
 

Makubwa haya, atoke ukristo aingie ukristo? naona ni kama kuruka ... kukanyaga...

Halafu mkatoliki, ni Insha Allah.
 
Kaa chini na wazazi wako waeleze kwa ufasaha kua huyu ndo mke uliemuona na uwaambie amekubali kubadil dini na waambie umempenda yeye na huna mwingine.

Wazaz wako sio watakao kaaa na huyo binti ni wewe mwenyewe hivo.jukumu la kutafta mke bora lipo mikononi mwako, wazaz wanatakiwa kua washaur na sio kuchagua yupi bora kwao
 
Dini si tatizo what matter ni tabia manake unaweza kupata huyo msabato na bado akawa tatizo...ur lucky unamjua vizuri na yupo tayar kubadilisha what else do u Need, wazaz huwa wanawaza mengi watoe hofu oa chaguo lako
 
Mkuu wazazi hawana mamlaka ya kubadili au kumtoa ,kuongeza mwenzi wako wa maisha wao watasaidia tu kuboresha ili kuyafanya maauzi yako yakae vizuri km bmk ilivyotakiwa lifanye. Madhara ya kubadili ni makubwa sana kwn ww na yy mtaachana na wazazi wenu na kuambatana na mke/me na kuwa kitu kimoja.

. One way of achieving more is to love what you have
 
Hiyo ni kubadilisha dini au dhehebu? Maana dini yenu ni moja (Wakristo) ila tofauti yenu ni madhehebu. Ni vyema ukae na wazazi wako mliongelee ili jambo kwa kwa kina mchumbako na wazazi wako wote ni wa muhimu.
 

Hamia katoliki funga ndoa achana na wazazi vilaza. Yesu ni yuleyule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…