Kigamboni planning authority

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI DARAJA LA KIGAMBONI

Thursday, September 20, 2012



* Aonya 'wenye viwanda' vya kutunga uongo kuacha tabia hiyo na kuelekeza nguvu kwenye maendeleo
* Asema viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kupigania maendeleo, wapo tayari nchi iyakose
*Asema tukio la kuwekwa jiwe la msingi ujenzi huo, leo litawanyima usingizi badala ya kufurahi

DAR ES SALAAM, TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 20, 2012, ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, huku akiwaonya watu ambao amewaeleza kuwa wanavyo viwanda vya kutunga uongo kuacha tabia hiyo na kuelekeza nguvu kwenye maendeleo.


Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wakazi wote wa Kigamboni ambao wanaondolewa katika maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa daraja hilo na ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni kuwa watalipwa stahili na haki zao zote.


Daraja hilo la Kigamboni ambalo wazo la kujengwa kwake lilibuniwa kwa mara ya kwanza zaidi ya miaka 30, tokea mwaka 1978, wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, linajengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 214.6 na litakuwa tayari katika muda wa miezi 36 ijayo, ingawa muda huo unaweza kupungua na kubakia miezi 30.


Daraja hilo ambalo litakuwa na urefu wa mita 680 linagharimiwa kwa pamoja na Serikali na Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF ambalo litachangia kiasi cha asilimia 60 na Serikali asilimia 40.


Daraja hilo ambalo litakuwa na barabara sita za kupitisha magari kwa wakati mmoja linajengwa na kampuni mbili za China ambazo ni China Railway Construction Engineering Group na China Railway Major Bridge Engineering Company na mhandisi msimamizi wa ujenzi huo ni Kampuni moja ya Misri.


Daraja hilo linatarajiwa kupunguza adha ya usafiri kati ya Kigamboni na Dar es Salaam ambao kwa sasa unategemea vivuko au boti ndogo, mitumbwi ama wenye magari kulazimika kufanya mzungumo wa kilomita 52.


Kwa uamuzi wa sasa, wavuka kwa miguu ambao watakuwa na njia maalum kwenye daraja hilo pamoja na waendesha baiskeli watavuka bure bila malipo yoyote.


Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali haiwezi kudhulumu wananchi wake na hivyo watu wote ambao wanastahili fidia kutokana na ujenzi wa daraja hilo na mji mpya wa Kigamboni watalipwa haki na stahiki zao.



Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake haitaruhusu mtu yoyote kuzuia ama kuchelewesha miradi ya maendeleo ambayo inalenga kunufaisha watu wengi.



Haya yaweza kuwa kejeli kwa madai ya msingi ya wanakigamboni kuwa Sheria haijafutwa na wao kama waathirika na miradi hii hawajahusishwa katika mchakato unaoendelea.
Hakuna mwanakigamboni wanao pinga mradi bali madai yao ya msingi kuhusu masilahi yao kulindwa hayajapewi nafasi.
Haijalishi imetajwa kuwa ni Bush anataka kununua au la!,lakini ukweli ni kwamba wakaazi watarajiwa wa huo mjipya ni wa aina ya BUSH na hata mpango uliopo kwa mujibu wa Ramani unasomeka hivyo kwa kuwa Wakaazi waliopo watahamishwa na Kupelekwa Zoo(Eneo tengefu Karibu na Kibada ili kuwapisha wanene.

Uhalisia wa mpango na ujenzi na majengo yanayotarajiwa kujengwa Kigamboni kwa mujibu wa Mpango wenyewe hata mtoto wa darasa la tano anaweza kung`amua kuwa familia yao haitaweza kuishi maisha ndani ya mji kama ule na kwa maana hiyo wanaona wazi wao lazima waondoke na kwamba kutakuwa na mtu mwingine atakaye kuja kuishi humo(Kigamboni new City)

Wanakigamboni wanataka zoezi zima lifuate sheria na liwe zoezi la wazi na washirikishwe hatua kwa hatua na lisiliwe suala la kisiasa kama Raisi anavyotaka lionekane na madai ya msingi wanakigamboni yaonekane ni hoja dhaifu .

Mapungufu yanazunguka zoezi hili la Mjimpya yamefanyiwa dokezo na Haki ardhi na ingependeza Raisi akapata muda wa kupitia na kufanya mlinganisho na anachoelezwa na wataalamu wa wizara pamoja na waziri mwenyewe(Prof.Tibaijuka).
View attachment THE NEW KIGAMBONI CITY, PROSPECTS AND CHALLENGES(6) 2012.pdf



Rais pia amesema kuwa wapo watu ambao hawapendi maendeleo ya nchi. “Wanatamani kila siku tushindwe kuwaletea wananchi maendeleo.
Maendeleo bila kutenda haki si maendeleo.Tatizo Serikali imebaki kuabudu miungu watu (Wawekezaji)na huku baadhi ya maofisa wakiona Kigamboni mahala pakustaafia kimasilahi kwa kushiriki kwenye uporaji wa Ardhi kwa bei poa na kwa jina la Uwekezaji.
Suala la kuwahamisha watu na kusema unawaletea maendeleo si haki hata kidogo.
Mradi huu ungependeza na wala usingekuwa na Kelele kama Serikali itabaki na Suala la Miundo mbinu na ikawashirikisha watakao athirika na miundo mbinu hiyo na hao wanaowaita wawekezaji wakabaki wanakubaliane na wenye maeneo/ardhi kwa upande mwingine KDA inayotaka kuundwa ikawa msimamizi ilikulinda haki ya Wenye Ardhi na pia kusimamia ujenzi unaoendana na Mpango Wenyewe.

Lakini watakufa kwa kihoro kwa sababu hatutashindwa. Kila tulilosema tutalifanya, litafanyika”.


Amesema kuwa thamani kubwa ya vyama vya siasa ni maendeleo ya wananchi. “Lakini wapo wenzetu ambao wanaudhika wakiona maendeleo. Wanapenda hata daraja hili lisijengwe. Leo hawatalala usingizi. Kazi ya vyama vya siasa ni kuweka maslahi yetu sote mbele.”


Posted by Bashir Nkoromo at 7:43 AM 0 comments Email This
 
Kaka umeongea vizuri zaidi, mimi nikiwa mmoja wa waathirika ki ukweli sijui undani ya mpango huu, naambiwa nitashirikishwa how? je nitaweza kumudu kuishi mji huo mpya na wanangu wakati kipato changu ni chini ya dola moja kwa siku? mji unaojengwa ni kwa ajiri ya wafanyabiashara matajiri, viongozi wa serikali na watu maarufu au ni wetu sisi watu maskini tunaomiliki maeneo haya?

Je wananchi hawa ambao JK alikuwa anawahutubia watakwenda kuishi wapi? maana nina uhakika hawataweza kuishi na wazungu katika mji huu mpya wa kihistoria.
 
Tuendelee kupata maoni ya wananchi mbalimbali.


 
 
Mkakati wa kudhulumu ardhi za walala hoi unaendelea.Serikali katika kutimiza ndoto yake ya kuwa dalali wa Ardhi kwa mwaka huu 2013 taarifa za chini chini zinadai wizara inapanga kupandisha gharama ya kufungulia madai ya kudai haki mbele ya chombo kinachotoa haki.

Jisomee mwenyewe na hii yaweza kuwa maandalizi ya kufanyikisha mambo mengine yaliyonyuma ya pazi toka kwa Serikali Sikifu !


[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 668"]
[TR]
[TD="width: 730"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD]
Gharama za ardhi kuwaliza wananchi
jumamosi, 5 januari 2013

na Edson Kamukara


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 730"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD] WANANACHI wa kawaida wenye vipato vya chini huenda sasa wakaikosa haki yao ya kufungua madai ya ardhi au makazi kutokana na serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupandisha mara dufu ada za kufungulia mashtaka hayo.

Tayari viwango hivyo vipya vimeanza kutumika kuanzia mwaka huu wa fedha hatua ambayo wadau wa masuala ya ardhi wanadai kuwa ni mkakati wa serikali kujaribu kuwazuia wananchi wa kipato cha chini kuufikia usawa huo kisheria.

Wadau hao wanasema kuwa hata awali kabla ya ada za kufungulia mashitaka kupanda, bado watu wa chini walikuwa wakishindwa kupata fedha za kufungulia madai yao hali iliyosababisha wengi wao kuamua kumuachia Mungu awapiganie.

Kwa mujibu wa gharama mpya, fomu ya maombi itapanda kutoka sh 500 hadi 4,000 wakati kufungua madai ya mali isiyozidi sh milioni 10 mwananchi atapaswa kulipia sh 40,000 badala ya 5,000 ya awali.

Kufungua madai ya mali inayozidi sh milioni 10, mhusika sasa atagharimika sh 120,000 badala ya sh 15,000 za awali, huku kupeleka hati ya utetezi kwa maandishi malipo yake yamepanda kutoka sh 2,500 hadi sh 20,000.

Gharama hizo zinaonesha kuwa, wale wanaotaka kufungua maombi madogo watalipia sh 40,000 badala ya sh 5,000 na kupeleka hati ya kiapo itakuwa sh 12,000 badala ya sh 1,500 za awali.

Kuingiza viambatanisho vya utetezi kwa kila kimoja gharama yake itakuwa sh 4,000 badala ya sh 500 wakati kufungua rufaa kutoka Baraza la Kata kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba sasa imepanda kutoka sh 2,000 hadi sh 16,000.

Mwananchi atakayetaka kupata nakala ya mwenendo wa kesi kila kurasa atagharamika sh 4,000 badala ya sh 500 na kuchukua nakala ya hukumu atalipia sh 16,000 badala ya sh 2,000 ya awali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, nakala ya amri ya Baraza inapanda kutoka sh 500 hadi 4,000 na malipo ya mpeleka hati ya madai, maombi madogo, hati ya kiapo, ama hati ya utetezi sehemu ya jiji au manispaa yameongezeka kutoka sh 3,000 hadi 24,000.

Malipo ya mpeleka hati ya madai, maombi madogo, hati ya kiapo, ama hati ya utetezi katika sehemu nyingine yoyote isiyo ndani ya jiji au manispaa yameongezeka kutoka sh 2,000 hadi 16,000 wakati kutoa maombi ya shahidi itakuwa sh 4,000 badala ya 500.
Kufungua gharama za kesi, mdai atapaswa kulipia sh 40,000 badala ya 5,000 ya awali na kufungua maombi ya utekelezaji ya hukumu imepanda kutoka sh 2,000 hadi 16,000.

Nazo gharama za kufungua/kupata hati/maandiko yoyote ambayo hayakuoneshwa katika utaratibu huu zitaongezeka kutoka sh 500 hadi 4,000.
Mjadala sasa unabaki kuwa pamoja na ada ya awali kuwa ndogo, bado walikuwepo watu waliokuwa wakishindwa kupata fedha za kulipia ada za kufungulia mashauri yao katika mabaraza. Sasa je kama hali ilikuwa hivyo kwa sasa itakuwaje?

Ni wazi kuwa gharama hizo zitakuwa zinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 24 (1) ambayo inamruhusu kila mtu kuwa na haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi kwa mali aliyonayo.


Juhudi za kupata kauli ya Wizara ya Ardhi, hazikuzaa matunda jana licha ya msemaji wake kusisitiza kuwa wanaandaa taarifa ya ufafanuzi, lakini hadi tunakwenda mitamboni hakukuwa na majibu yoyote.





[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mhe.Tibaijuka.
Wakati Wizara inaota ndoto ya Kufanikisha mji Mpya wa Kigamboni inatakiwa kuweka wazi masilahi na thamani/viwango vya malipo kwa kwaazi watakaoathirika na mradi kwa kutumia thamani/msukumo wa Soko.
rejea baadhi hapo chini kama kianzio.


Hii kwa hesabu za haraka One square Meter. 900,000,000 /1540= 584,415.6tzs na eneo hii liko kilomita kadhaa na pwani.




Je waathirika kama hawa kweli Serikali imejianda sawa kukabiliana na matatizo haya na ni lazima kiasi kama hiki cha pesa kutumika wakati tuna miradi mikubwa yenye kuhitaji pesa kwa haraka mfano Umeme,Hospitali ,Elimu na mengine mengi ambayo ni aibu kufikiri na kutumia trilioni kadhaa kujenga mji.

Serikali ingeishia katika hatua ya Kutoa Ramani/Muundo wa Jinsi Mji utakavyo kuwa na Kuiachia Halmashauri husika ikishirikiana na City Council suala la Usimamizi wa Ramani husika huku Taasisi binafsi ,Mtu mmoja Mmoja au Taasisi za Umma kama (NHC) zenye kufanya Uendelezaji Majengo ichangamkie Kazi hii.
 
Hii ndiyo Serikali sikifu.Na haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania.
Kama kweli maendeleo ni kwa staili hii siamini wanaoimba kwamba wanataka kuwa nufaisha wakaazi wa maeneo husika ni ya kweli.

Kwa Serikali inayoamini utawala wa Sheria ingewapeleka mahakamani wahusika na sikuvunja Nyumba zao.
Je walikuwa na hati ya mahakama ?
 
Suala la Mtaa wa Minondo, Somangila, Kigamboni

Wahusika wa wakuu wa unyama huu na ufisadi ni

Sadiq Meck Saidiq mkuu wa mkoa wa Dar,

Said Mwema, mkuu wa jeshi la polisi,

Mkuu wa wilaya ya Temeke,

Diwani wa Somangila almaarufu Mama Mpanjila


Hawa wamepigwa milioni 800 na mchina, wakauza ardhi ya wananchi kwa mgongo wa mji mpya wa kigamboni
 

Mkuu funguka kidogo ili wadau waelewe unyama wanaofanyiwa na viongozi wao kwa Tamaa za fedha na mali kupitia kwa jasho la walalahoi.

 



Mkuu habari hiyo inatisha.Je Ni Mchina wa Kampuni gani hiyo ?

Kweli naanza kuamini msemo wa serikali hii ni ya CHUKUA CHAKO MAPEMA-CCM
 
Hii ndiyo serikali kweli ni maajabu kwa kauli kama hii kutoka kwenye kinywa cha waziri tena profesa.
Haya ndiyo baadhi ya mambo tunataka Katiba Mpya iyatamke kuwa ni kosa na mhusika lazima awajibishwa au ajiwajibishe au aombe radhi.

Hivi kwenda Mahakamani ni kudanganyana? na Kama wanadaganywa siasubiri huo udanaganyifu!


[h=3]Prof Tibaijuka: Hameni Mivinjeni[/h]
 
Taarifa zilizopo zinadai Kamati ya Ardhi ,Maliasili na Mazingira chini aJames lembeli itakutana na Kamati za Tibaijuka kuhusiana na Mji Mpya wa kigamboni .

Lakini kinachosikitisha Kamati ya Lembeli imekwepa kukutana na Kamati Kubwa ya Waakazi wa Kigamboni ambayo imekwisha kutana na Kamati hii ya Lembeli lakini safari hii inaonekana ujio wao eneo la Kibada na kuja kuonana na Kamati za mitaa zilizoundwa kupitia Waziri Tibaijuka pamoja na Wizara yake kwenye Mradi huu wa Mji Mpya na wakiwa walalamikiwaji inaleta shaka .

Kamati ya Lembeli kama kweli inakwenda kufanya kazi ya Uwakilishi wa Umma/Watanzani ingefanya pia jitihada ya kuonana na Kamati yenye kuwakilisha Masilahi ya Wakaazi Wengi wa Kigamboni
 
Asante Mhe.Mbunge.
Ujumbe huu umetulia ni wale wasiopenda haki ikitendeka ndio waanoweza kuziba masikio yao!


 
Hivi kuna nini kinaendelea, mwenye info kama hii KDA imeshaanza kazi rasmi kisheria ya kuendeleza mradi huu hasa kuanza kulipa fidia wahanga wa ardhi watakaopisha ujenzi wa mji huu wa kisasa.
 
Hivi kuna nini kinaendelea, mwenye info kama hii KDA imeshaanza kazi rasmi kisheria ya kuendeleza mradi huu hasa kuanza kulipa fidia wahanga wa ardhi watakaopisha ujenzi wa mji huu wa kisasa.


Mkuu FUSO hao jamaa wako kazini tayari na wanaofisi Kigamboni. Ukitaka kuwa tembelea Ofisi yao iko karibu na Beach moja inaitwa Mikadi Beach ukifika hapo ulizia na kama unamacho mazuri utaona Kibao chao.

Na kwa taarifa Kibada maeneo ya Uvumba na Kivurugwe wamekwisha anza kuchakachua ardhi za wenyeji .
 
Last edited by a moderator:
we are excellent on papers, but utendaji nehi che

Kigamboni ni a very good sign on how inefficient and unproductive serikali imekua kwenye maeneo nyeti kama ardhi

kinachotakiwa ni executive order na kuanza implementation, in addition, serikali haiwezi na haipaswi kutekeleza transformation ya kigamboni, inatakiwa iandae sera, mipango na miongozo halafu iache private sector i drive the implementation
 
Haya naona kimya kimekuwa Kingi ni vizuri tukakumbushana .Mwaka umepita sasa hivyo wakati Bajeti ya Wizara husika ikiwa ni
NEW: PARLIAMENT TIMETABLE Click here to Download
21.JUMAMOSI 31/5/2014 • HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO
YA MAKAZI. Saa 3.00 Asb – 7.00 Mchana NA Saa 10.00 Jioni - 2.00 Usiku

kwa wale waathirika wa Mradi huu ni vizuri waka tega masikio vizuri !.

Maana hayo yaliyoahidiwa na Mhe.Tibaijuka ni mwaka umepita ,lakini pia ni miaka zaidi ya Mitano toka Mradi utangazwe na hakuna cha Maana kinachoendelea zaidi ya Kuundwa Taasisi na kuwapa Watendaji Ulaji.

Wabunge wetu Mpoo!!!!!!!!!.



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…