Kigamboni planning authority | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigamboni planning authority

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by Mp Kalix2, Jan 10, 2011.

 1. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  wana Jf. Kwa heshima kubwa naomba msaada kwa yeyote mwenye kuona ,kufahamu kuhusu rasimu ya Mamlaka hii. Mimi ni mdau mwathirika na mradi wa Mji-Mpya wa Kigamboni. Kuna hii habari ya kuundwa kwa mamlaka ya kusimamia huu mradi kama ilivyokuwa CDA(Dodoma) Hivyo wadau waathirika tunafaa kushirikishwa katika uundwaji wa hii Mamlaka maana ndiyo itakayo simamia ,kuendesha na kushughulikia matatizo yote yatakayotokana na huu mradi, bahati mbaya wahusika mpaka sasa wako kimya. Lakini chakushangaza zaidi mpaka sasa wizara husika haijafanya mawasiliano au kutoa taarifa kwa walengwa kujua nini kinaenedelea kuhusu huu Mradi pamoja na kwamba NOtisi imekwisha expire 24/10/2010. Habari hii unaweza kuisoma hapa. A dream behind the plush Kigamboni By Stella Barozi 31st May 2009 SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY Kuongezea nyama zaidi.

  Update;24/1/2013
  Huku ndiko kuziba masikio.Au unaweza kuita Serikali sikivu.

   
 2. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sijaluelewa, notisi umekwisha wewe unataka serikali ikuambie nini? Wewe ni ccm ulikuwa unasubiri ulaji kupitia kamati? Watu wanashukuru shetani kapita wewe unatonesha vidonda?
   
 3. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  Heshima yako Mkuu.
  Nilitegemea baada ya Notisi hatua zingine muhimu husika na Mradi inaanza ikiwa pamoja na kuwa fahamisha wahusika/waathirika.Hofu yangu Kubwa ni mambo kama ya watu wa Kipawa(Airport DSM) wamekaa kwa miaka 12 wakisubiri tu mradi uanze na walipwe kwa wale watakao athirika.

  Mkuu kama wewe ni moja wapo wa waathirika mtarajiwa usiote ndoto ya mchana kuwa shetani kapita labda kama unawapotosha watu kwa manufaa yako,kama wengine wanaopita Mtaani wakiwa tapeli watu kuwa Mradi haupo tena na wanawashawishi watu kuuza ardhi zao.

  Narudia tena kwa Wana JF wenye nafasi ya kuwezesha sisi waathirika kuweza kuiona/kupata Rasimu ya Uundwaji wa Hii Mamlaka inayotarajiwa kuundwa kusimamia Mradi huu wa Kigamboni.

  Nadhani wengi wana fahamu au wamesikia kinachofanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma.Kuna malalamiko wengi toka kwa wakaazi wa Mji wa Dodoma kuhusu mamlaka na hii ni kwasababu Mamlaka haijashirikisha wahusika wa Ardhi/waathirika hivyo hata hii ya Kigamboni wisho wake utakuwa kama hii ya CDA ndiyo maana ni muhimu wadau/waathika kushirikiwa toka mwazo wa uundwaji wake.


   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Danganya toto ile!Utasubiria mpaka uzeeke!
   
 5. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  Up dates;
  Kigamboni imekufa kabla ya kuanza
  Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 25 May 2011
  Jamvi la Weledi
  KASHFA nzito ya ardhi imeibuka Kigamboni jijini Dar es Salaam inayothibitisha usemi kwamba "penye fedha na ardhi viongozi wa chama tawala (CCM) na watendaji wake serikalini hawana haya."
  Tulikiona kilichotokea kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania. Kila mwenye jina katika CCM, alijichotea.
  Uhuni wa kupora fedha za EPA sasa unajirudia na unatekelezwa Kigamboni wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Tofauti na huko nyuma walipokuwa wanapora fedha, sasa wanapora ardhi ya wakazi wa Kigamboni kwa kisingizio cha kujenga mji mpya.
  Mgogoro uliopo ni kwamba watawala hawataki kabisa kufuata sheria zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi huo. Hapa sheria zinazohusika ni Sheria ya Utwaaji wa Ardhi Na. 47 ya mwaka 1967 na Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya mwaka 2007.
  Walianza kwa kuutangazia umma mwaka 2008 kuwa kungejengwa mji mpya Kigamboni na wakazi wake wakazuiwa kuendeleza, kwa namna yoyote, ardhi yao hadi hapo watakapolipwa fidia ili kupisha ujenzi wa mji huo.
  Tangazo la serikali la 24 Oktoba 2008 kwenye gazeti la Serikali Na. 43 Vol. 89 lilikuwa na taarifa ya amri ambayo ilianisha mipaka ya eneo litakalokumbwa na ujenzi wa mji mpya kuwa ni kata tano za Somangila, Kigamboni, Vijibweni, Kibada na Mji Mwema.
  Amri ya serikali ilionyesha waziwazi kuwa ilifanyika chini ya kifungu cha 34 cha Sheria ya Utwaaji Ardhi sura ya 118 ambayo inahusu upangaji vizuri na ujenzi wa makazi tu na siyo viwanda, maofisi na maghorofa ya taasisi za umma.
  Sheria hii ya utwaaji wa ardhi inarahisisha sana utwaaji ardhi kwa ajili ya kuwapanga vizuri wakazi wanaoishi katika makazi holela, yasiyo na miundombinu mizuri kama barabara, maji, umeme, vituo vya afya, shule na majumba ya maendeleo.
  Sheria hii hairuhusu watawala kuleta watu wengine ili kuwaendeleza kwa kisingizio chochote kile hata cha uwekezaji. Ardhi ikitwaliwa chini ya sheria hii itagawanywa kwa wakazi walewale waliokuwapo baada ya kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya miundombinu.
  Lakini kama lengo la kutwaa ardhi ni kwa ajili ya maendeleo, basi sheria husika inayotakiwa kutumika ni Sheria ya Mipango Miji namba 8 ya mwaka 2007. Sheria hiyo inawapa mwanya wa kuchukua maeneo na kugawa inayobaki au kuwaleta marafiki, wawekezaji na wengi wengine.
  Watawala wa CCM hawataki kutwaa ardhi chini ya sheria hii kwa sababu ina masharti magumu. Masharti hayo ni pamoja na kulazimisha uwazi na ushirikishwaji wananchi katika kuendeleza ardhi husika.
  Kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinataka kabla ya kutangazwa eneo kuwa eneo la kuendelezwa, kwanza wananchi waelezwe na waukubali mpango/ mradi huo.
  Jambo hili halikufanyika Kigamboni kwa sababu sheria iliyotumika kutwaa ardhi yao siyo ya kutaka kuendeleza, bali ya kutaka kuwapanga wakazi waliojenga holela ili sasa nyumba zipangwe kwa mitaa na miundombinu iwekwe.
  Kifungu cha 11 cha Sheria ya Mipango Miji kinataka mamlaka husika kutayarisha rasimu ya uendelezaji huo ndani ya miezi sita kwa ushirikiano na wadau wote wakiwamo wamiliki wa ardhi kwa maana ya wananchi hasa wakazi wanaomiliki nyumba Kigamboni. Hili halikufanyika kabisa.
  Kifungu cha 19(3) kinazuia uendelezaji wa eneo lolote chini ya Sheria ya Mipango Miji kama utaratibu uliowekwa na sheria hiyo (kuanzia kwenye tangazo, uandaaji rasimu na upitishaji rasimu ulioainishwa katika vifungu 8 – 18) haukufuatwa.
  Pamoja na kwamba watawala wamekiuka sheria kwa kutwaa ardhi wakitumia sheria tofauti na sheria inayotakiwa kwa ajili ya uendelezaji wa ardhi ya Kigamboni, bado wamepanga awamu tatu za uendelezaji ardhi hiyo utakaotekelezwa katika miaka 20 tangu 2011 hadi 2030.
  Awamu ya kwanza imepangwa kuanza 2011 hadi 2020 ambapo yatajengwa madaraja na barabara na ujenzi wa nyumba 16,000 kutosheleza watu 100,000 kabla ya mwaka 2014; awamu ya pili 2021 hadi 2025 na awamu ya tatu ni 2026 hadi 2030.
  Maswali yanayokuja ni mengi. Kwanza mbona mpango huo haukufuata Sheria ya Mipango Miji ya mwaka 2007? Mbona utekelezaji wake umeanza kabla ya kupitishwa mpango kamambe (master plan)?
  Je, wananchi watakaaje tangu 2011 hadi 2030 bila fidia, bila kutumia ardhi yao kama dhamana kukopa, bila kuendeleza nyumba zao? Mbona mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile yeye amejenga bila kuhojiwa? Mbona orodha ya wakazi haitangazwi wakati tunajua wameorodheshwa wasiokuwapo Kigamboni?
  Kwa nini wananchi wa Vijibweni wanahamishwa eti ili kupisha upanuzi wa bandari wakati eneo hilo lipo ndani ya mradi? Je, mamlaka ya uendelezaji mradi wa mji mpya Kigamboni (Kigamboni Development Authority) ndiyo inayowahamisha?
  Kama ni KDA mbona utaratibu tulioahidiwa wa kujengwa maghorofa ili wananchi wakihamishwa wakae haufuatwi? Maghorofa tuliyoahidiwa na Waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka, hayajajengwa sasa hawa wananchi watakwenda wapi?
  Kumbukeni KDA ndiyo yenye jukumu la kuhamisha na kutoa makazi kwa wananchi wakati ahadi ya Rais Jakaya Kikwete alipotembelea Kigamboni kabla ya uchaguzi ilikuwa "hakuna mtu atakayehamishwa bali mtasogezwa kupisha miundombinu."
  Mbaya zaidi serikali inatangaza kwamba eti itawavunjia wale waliojenga baada ya amri ya zuio wakati yenyewe haisemi kuhusu jinsi ilivyokiuka sheria yenyewe na kitu gani kitafanywa kwa wakubwa waliokiuka sheria makusudi kuhakikisha wanapata ardhi Kigamboni.
  Historia ya mradi huu ni ndefu tangu tulipotangaziwa 2008 kuwa mji huo mpya wa Kingamboni ungekuwa wa kisasa wenye maghorofa kedekede, barabara pana kama Ulaya, madaraja mawili moja Kurasini na jingine Magogoni usawa wa ikulu pamoja na maeneo ya viwanda, burudani na mahoteli ya kitalii.
  Kwa kufahamu tabia za viongozi na watawala wetu kila mahali penye fedha na ardhi wananchi wa Kigamboni walianza mara moja kupiga kelele wakidai Kigamboni imeuzwa ili CCM wapate fedha za uchaguzi wa 2010. Wananchi hawakusema Kigamboni ilikuwa imeuzwa kwa nani.
  Wa kwanza kufika Kigamboni kuwatoa shaka wananchi ni aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ambaye pia alikuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati akisema wananchi hawatahamishwa bali watajengewa maghorofa ndani ya Kigamboni wakae.
  Chiligati alifuatiwa na Rais Kikwete ambaye alihutubia umati akikana Kigamboni kuuzwa na kusema ni mradi wa kuboresha makazi huku akisisitiza "hamtahamishwa ila mtasogea tu kupisha ujenzi wa miundo mbinu basi." Kikwete alitangaza pia kujengwa barabara ya Feri – Tungi kwa kiwango cha lami.
  Walipotembelewa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa sasa, Anna Tibaijuka, wenye mabango ya kuonya uchakuachuaji ardhi yao wakakamatwa na polisi kwa amri ya diwani wa Kigamboni, Doto Masawani. Haya yote ni ushahidi tosha mradi haupo au umekufa.
  0785788727, kicheere@yahoo.com
  Source.
  www.mwanahalisi.co.tz
   
 6. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  Habari zenu wanajamvi. Taarifa kwa wakaazi Kigamboni na wengine wote wenye Interest na Mradi wa Kigamboni.Kuna uwezekano wa kuwa na Mjadala kuhusu mradi husika kwenye moja wapo ya TV station zetu za Bongo kuanzia saa Tatu Nusu Usiku siku ya Jumamosi.17/12/2011
   
 7. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  Habari zenu wanajamvi. Taarifa kwa wakaazi Kigamboni na wengine wote wenye Interest na Mradi wa Kigamboni.Kuna uwezekano wa kuwa na Mjadala kuhusu mradi husika kwenye moja wapo ya TV station zetu za Bongo kuanzia saa Tatu Nusu Usiku siku ya Jumamosi.17/12/2011


  Up dates.
  Kutakuwa na kipindi pia kati ya saa Nne hadi saa Tano usiku.Vipindi vyote hivi vitakuwa kwenye Tv mbili tofauti ili kutoa nafasi kwa wale watakao kosa ile ya saa Tatu na nusu.
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ni wazo zuri ngoja nimstue naye ni mhanga..
   
 9. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu.Si vibaya hata kama si mhanga wa leo anaweza kuwa wa Mhanga wa Kesho.

   
 10. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  [h=1]Tibaijuka anatumika kuhalalisha uporaji ardhi Kigamboni[/h][HR][/HR]

  Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 07 December 2011

  Waraka wa Wiki  KILA George Walker Bush, yule mtangulizi wa Rais Barrack Obama katika Ikulu ya Marekani, akitembelea Tanzania, wakazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam huwa matumbo moto huku viongozi wa CCM na serikali, bila kuulizwa, wakihaha kukanusha kuwa Bush hakufuata ardhi yao.
  Hayo ndiyo yaliyotokea wiki iliyopita, rais huyo wa zamani wa Marekani alipotembelea Tanzania ghafla, huku watu wengi wakiwa hawana habari. Katika hali ya ughafla huo huo, zikajitokeza taarifa kuwa anafuatilia ahadi aliyopewa na serikali kuhusu ardhi ya Kigamboni.
  Pamoja na serikali kuwahi kukanusha mapema katika miaka ya 2008 na 2009 kuwa Kigamboni haijauzwa kama inavyotangazwa na wambeya, bado swali moja linahitaji majibu. Kwa nini kila mara ajapo Bush nchini pirikapirika za mradi wa Kigamboni hufufuka?
  Mara ya kwanza alipotembelea Tanzania, wakati huo akiwa bado rais wa Marekani, aliporejea kwao tu, huku nyuma ikatangazwa kuwa kutaanzishwa mradi mkubwa wenye thamani yaa matrilioni ya shilingi eti wa kuuendeleza mji wa Kigamboni. Hawakusema pesa hizo zingetoka wapi.
  Ikaandikwa magazetini, ikatangazwa redioni na kwenye televisheni, kuwa mradi huo ni wa Bush na kwamba ni matayarisho ya kuwekwa kituo kikubwa cha kijeshi cha nchi hiyo kiitwacho African Command. Serikali ilikanusha vikali lakini hakuna aliyeamini.
  Wiki iliyopita tena Bush katembelea nchini bila taarifa kuwafikia watu wengi na ghafla zikazuka taarifa za Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kuanza ziara maeneo ya Kigamboni, katika awamu ya mwisho ya kuutangaza mradi huo wa uendeleazaji Kigamboni.
  Kulingana na ratiba iliyotolewa, waziri Tibaijuka alitarajiwa kutembelea na kufanya mkutano katika viwanja vya Machava Kigamboni jana, na leo anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa Vijibweni juu ya mradi huo wa kuendeleza Kigamboni iwe kama Dubai.
  Namna mradi huu ulivyoandaliwa, ulivyojulishwa kwa wananchi na namna utekelezaji ulivyoanza, inadhihirisha wazi kuwa ni mradi wa uporaji ardhi za wananchi Kigamboni na siyo mpango wa mji mpya kama inavyoelezwa.
  Zipo sababu nyingi za kuhalalisha msimamo wa wananchi kuwa wanaibiwa ardhi zao kwa kisingizio cha mradi wa mpango wa mji mpya Kigamboni, na hapa tutataja sababu chache tu kuonyesha unafiki wa viongozi wa serikali na watendaji wa wizara ya ardhi.
  Kwanza, kutokana na sababu zisizofahamika, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Joseph Ole-Medeye, aliongopa waziwazi bungeni pale alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungulile.
  Akijibu swali, katika mkutano uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, Naibu waziri huyo alisema wananchi wa Kigamboni walishirikishwa kikamilifu katika kuandaa mpango huo wa Mji mpya Kigamboni eti nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kata kwa kata!
  Haieleweki ni wananchi wangapi Kigamboni walishirikishwa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kata kwa kata! Nijuavyo mimi, wananchi hawa waliunda kamati yao wakaiandikia wizara barua nyingi, si chini ya sita, wakati wote huo wakitaka kuhusishwa katika mchakato wa mradi, lakini hawakupewa majibu yoyote.
  Ikafikia hatua Katibu mkuu mpya, Patrick Rutabanzibwa alipohamishiwa wizara ya Ardhi, ujumbe wa kamati hiyo ya wananchi Kigamboni ulimfuata ofisini kwake ukitaka kushirikishwa, naye akawaamuru watendaji waliokuwepo akiwemo Mratibu wa Mpango na Mkurugenzi wa Mipango Miji, wajibu barua za kamati.
  Nakala za barua za kamati zilizotumwa wizarani kuomba kushirikishwa zipo, na majibu ya wizara yaliyotumwa kwa lazima baada ya Rutabanzibwa kuwaamuru watendaji wake wajibu yapo. Sasa huko ndiko kushirikishwa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kata kwa kata?
  Pili wizara inadai eti haikuzuia wananchi kuendeleza ujenzi wakati wizara hiyo hiyo ilitoa matangazo magazetini ikipiga marufuku wananchi kuendelea kujenga ikidai eti wanajitakia hasara. Na leo hii katika majibu ya waziri bungeni serikali inadai vibali vinatolewa kuendeleza ujenzi!
  Wananchi sasa wanajiuliza, kama kweli serikali inatoa vibali vya ujenzi, leo Waziri anafanya ziara Kigamboni kuchukua maoni ya mwisho kabla ya kupitisha mradi, ni maoni gani anayokwenda kuchukua ikiwa vibali vinatolewa ili wananchi wajenge kulingana na matakwa ya mradi?
  Kwani kuna miradi mingapi? Na yeye waziri anakuja kuchukua maoni ya mwisho kulingana na tangazo la ujio wa Waziri kwani maoni ya mwanzo au ya pili aliyachukua lini au kiongozi gani aliyachukua maoni hayo na lini kuthibitisha kama wananchi wanautaka mradi wa mji mpya Kigamboni au la?
  Tatu na mbaya zaidi, daftari la uhakiki wa wakazi wa Kigamboni limeletwa kila mtaa likiwa na mapungufu makubwa na mengi zaidi kuliko hata mapungufu yaliyomo kwenye lile Daftari la Kudumu la Wapiga kura nchini.
  Daftari hilo la wamiliki ardhi Kigamboni linaonyesha majina mengi ya wamiliki ardhi hayamo, majina mengine ya wamiliki ardhi yamewekwa mitaa na kata tofauti na wanapoishi na kumiliki ardhi, maeneo yamegawanywa tofauti na uhalisia na mwisho majina mengi hayafahamiki na inadaiwa ni majina ya ndugu, marafiki na wapenzi wa watendaji wa wizara ya ardhi.
  Sababu ya nne, inayowafanya wananchi waamini kuwa huu ni mradi wa uporaji ardhi yao, ni namna uteuzi ulivyofanywa kwa kumfanya mbunge wao kuwa mwanakamati ya kuhami mradi! Kama mbunge ni mwanakamati wao, sasa wananchi wakalalamike kwa nani?
  Kwanza haikuwa halali kuteua kamati ya watu kumi, tisa kutoka nje ya mradi na mmoja kutoka ndani ya Kigamboni tena naye ni mbunge. Kumteua mbunge katika kamati hii ni kumziba mdomo na kama hivi ndivyo, nani sasa atawatetea wana wa Kigamboni?
  Hata uteuzi wenyewe haukufuata sheria hasa vifungu vya 8 na 9 vya sheria namba 8 ya mwaka 2007 ya mipango miji vinavyotaka wakazi wa eneo husika washirikishwe na wakubali bila hivyo mpango ni batili.
  Kwa Waziri Tibaijuka, aliyekaa Shirika la Maendeleo ya Makazi la Umoja wa Mataifa la Habitat miaka mingi, kukubali na kuingia kazini kuutetea mpango ambao ni batili, hayo ndiyo aliyokuwa akiyafanya Habitat, Nairobi?
  Waziri Tibaijuka alikutana na kamati ya wakazi Kigamboni bungeni Dodoma mapema mwaka huu wakati huo wakishinikiza washirikishwe katika mchakato wa mradi, leo anadirikije kuungana kuhalalisha mradi batili ambao hata ngumbalo akifungua kesi atashinda mahakamani? Ama kweli huu ni mradi wa kuhamishia Kigamboni wakazi wa Masaki, Oysterbay, Mbezi Beach na Mikocheni wenye uwezo wa kujenga maghorofa kumfurahisha Anna Tibaijuka na kutumia daraja linalojengwa kwa sababu wakazi wa sasa hawahitaji kutumia daraja wala pantone kubwa. WIZI MTUPU WA ARDHI

  Source.
  www.mwanahalisi.co.tz

  Note. Kunategemewa kutakuwa na Mjadala wa Mradi wa Mji pya wa Kigamboni kwenye TV mbili tofauti za hapa Bongo.Moja saa tatu na nusu mpaka saa Nne na mwingine saa Nne mpaka saa Tano wapenzi wote wenye kupenda mijadala mnakaribishwa.
   
 11. j

  joseph1983 Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa m2 makini kama anafikiri mbali zaidi kuliko viongozi we2 kwa nini kigamboni ikumbukwe leo?mgeni atoka marekani kuangalia saloon za kike pale magomeni kunanini?,kwanini wenyeji wa kigamboni waondolewe?,kwa nini leo tukadai kuongezewa mpaka baharini?ha2kuliona hilo hapo nyuma?je 2nafikiri umoja wa mataifa watakataa tanzania kiongezewa mpaka huo?.Haya mji wa kigamboni umejengwa tena kisasa(mega-city) ni nani atakaye ishi huko?kama watanzania wa hali ya chini wameondolewa huko tena kwa kupigwa danadana fidia zao na uongozi wa wizara ya arhi?
   
 12. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kigamboni yetu! Tuko roho juu
   
 13. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tuko roho juu mkuu, haieleweki, usubirie utie hela yani nchi yetu hii kuna baadhi ya mambo yanasikitisha kweli

   
 14. survivor03

  survivor03 JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 225
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  oyaa... usitishe watu, mbona mbunge wa kigamboni DKT. Faustine N. Amesema mpaka mwezi wa sita finaly hakuna cha mradi, kama issue ya mji mpya itakuwa kimya. Na usifananishe kigamboni sawa na kipawa. Unataka kusema wananchi tunaoishi sote kigamboni zaidi ya millioni tutanyanganywa nyumba zetu halafu basi,
  Hakuna cha kulipwa nyumba kutokana na tathmini ya nyumba wala nini? Mbona pointi yako haieleweki? Una maana gani?
   
 15. A

  Adili JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,008
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mradi wa Kigamboni ni mradi wa wachache waliowahi. Ni lini ulisikia taifa likifafanuliwa ni nini kinakusudiwa/kitatendeka/kinatendeka Kigamboni? Matayarisho ya yatakayotokea Kigamboni yatagharamiwa na mlipa kodi, ila huyo mlipakodi hapaswi kujua atagharamia nini. Ni watanzania wangapi wanaweza kuingia mtandaoni na kujionea serikari inafikiria kuigeuza vipi kigamboni?
  Watakaoathirika na mradi huu walijumuishwa vipi na watakuwa compensated vipi? Watanzania wa sasa tuna daraja tatu. Ya kwanza na juu kabisa ni "Hasante Mwinyi-Mkapa-Kikwete" , ya pili na kati ni "Hasante Mwinyi-Mkapa" na daraja lchini na mwisho na ndio wengi zaidi ni "Hasante Mwalimu".
  Huu mradi wa Kigamboni ni kwa manufaa ya daraja mbili za juu.
   
 16. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  Maendeleo kuhusu mradi wa mji mpya wa Kigamboni.
  Habari mpya kwa 2012.
  [FONT=&quot]Residents: Suspend Kigamboni project[/FONT]
  [FONT=&quot]By The guardian reporter [/FONT]
  [FONT=&quot]24th January 2012[/FONT]

  [FONT=&quot]Comments[/FONT]
  [FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]MP, Dr Faustine Ndugulile[/FONT]
  [FONT=&quot]A fresh row ensued yesterday between Kigamboni residents and authorities over implementation of a multi-billion housing project, which seeks to transform the area into a modern satellite city.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]The residents with the support of their MP, Dr Faustine Ndugulile want the government to organise public hearing before implementing the project.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]The residents’ reactions followed a letter from the government to Temeke Municipality which explained how the areas would be marked for installation of necessary infrastructures as part of the project implementation.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]They said they were ready to vacate the area to pave way for the project but wanted the government to hear their views first and educate them before implementation of the project, as stipulated in Section 19 of the urbanisation Act of 2007. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]In an exclusive with The Guardian, Chairperson of Kigamboni residents committee, Stewart Swai said the association does not oppose the project but needed to be involved in the implementation process.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]“Our expectations were that we would be involved at every step of implementation of the project, but the situation is now quite different,” he said.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Swai explained that the Minister of Lands, Housing and Human Settlement Development, Prof Anna Tibaijuka ordered the government officials to work together with the residents including his committee in the implementation of the project. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]“We are ready to work with them but they are going on with the implementation of the project without involving us,” he noted.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  Hii ndiyo serikali.Inafanya kazi ya udalali ya kununua na kuuza ardhi ya wakaazi wa Kigamboni kana kwamba wenye ardhi hawajui au hawana uwezo wakufanya kazi hiyo na hawajui thamani ya vipande vya ardhi wanazomiliki


  [FONT=&quot]Kigamboni legislator, Dr Faustine Ndugulile said he wrote a letter, with reference No.MB/AR/KNC/01/2012 of January 9, 2012 to Prof Tibaijuka, asking her to stop implementation of the project.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]“But I have not receive any response,” said the MP, saying he warned that implementing the project without landholders’ opinions was a violation of the law and that the process would be illegal.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Speaking to this reporter yesterday, the MP said: “This project is yet to get the residents’ blessings…that’s why there are so many shortcomings…for instance project drawings show that Kigamboni is empty land, which is not true.” [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]He added: “Even the names of landholders provided by the government are not correct…some of the names are missing.” [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Reached for comment yesterday, the Minister for Land, Housing and Human Settlements Development, Prof Tibaijuka stated that her ministry is in the process of setting up a system of collecting people’s views on the project.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]“Residents should not get worried because the project is the biggest in our country, thus we are still organising ourselves,” she clarified.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]She pledged that every resident will be compensated according to his assets, asking them to stay calm while the government worked on the modalities of implementing the project.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]The minister also allayed residents’ fears on the formation of KCDA, saying the authority would work closely with them in the processes of project implementation.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  Katika hili Waziri anawataka waakazi kusimamisha uendelezaji na kuita hatua ya uendeleza kuwa ni kuvunja sheria, lakini haelezi kivipi Wizara yake (Serikali)imevunja sheria katika hatua zote za maandalizi ya mradi huu;kutoka utoaji ya taangazo,ushirikishwaji wa waathika/wakaazi ambao kisheria wizara inatakiwa kuwashirkisha katika kila hatua ya mradi kwa kufanya mikutano ya hadhara kwa kila Kata na kukubaliana katika kila kipengele kinachohusiana na mradi wenyewe hasa katika mambo yafuatayo; aina ya mradi,manufaa ya mradi kwa wakaazi na taifa kwa ujumla, mipaka ya eneo la mradi,,malipo ya mali,malipo ya ardi,malipo ya usumbufu,eneo mbadala kwa watakao hamishwa,muda wautekelezaji,kanuni itakayotumika kufikia viwango vya malipo(hii ni lazima iwe kwa mujibu wa thamani ya Soko kwa muda huo wa kulipana, mambo haya na mengineyo lazima yakubaliwe na pande zote mbili kabla ya hatua yoyote ya utekelezaji wa mradi husika. [FONT=&quot]SOURCE: THE GUARDIAN ( http://ippmedia.com)[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
   
 17. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 1,152
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Mwendelezo wa Taarifa mbalimbali kuhusu Mji mpya wa kigamboni.
  Katika hali inayoonyesha kuwa baadhi ya viongozi wa Kisiasa wanataka kugeuza huu mradi kuwa mtaji wa kisiasa soma hapa chini kauli zao.
  Maofisa Ardhi watimuliwa kikaoni[/FONT]


  [FONT=&quot]By Moshi Lusonzo [/FONT]
  [FONT=&quot]7th April 2012.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Katika hali isiyotarajiwa maofisa wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi wamejikuta wakitimuliwa kwenye kikao baada ya Wabunge na Madiwani wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kukataa taarifa waliyoitoa kuhusu Mradi wa mji mpya wa Kigamboni na kuwataka wakatafute majibu ya uhakika.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Tukio hilo limetokea juzi wakati Madiwani hao wakiongozwa na Wabunge wawili, Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mariam Kisangi, Viti Maalumu walipohudhuria kikao maalum ya utekelezaji wa mpango wa mradi wa mji mpya wa Kigamboni iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Katika kikao hicho mtoa mada alikuwa mratibu wa mradi huo, Mganga Majura, ambapo katika maelezo yake alisema mradi huo umepangwa kuwa katika awamu mbili ikiwemo mpango wa kuandaa mradi ambao umekamilika na hatua ya utekelezaji wake inatarajiwa kuanza hivi karibuni.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, wakati akitoa mada hiyo pamoja na kuonyesha picha ya video ya jinsi mji huo utakavyokuwa, wabunge hao pamoja na madiwani walitaka kabla zoezi hilo halijaendelea wapewe ufafanuzi wa maswali manne ikiwa pamoja na lini mradi huo utaanza, wapi utaanzia, namna ya ulipaji wa fidia na nini hatma ya wananchi wa eneo hilo.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Aliyeanzisha sakata hilo alikuwa Mbunge Ndugulile, ambapo aliponyanyuka kuchangia mada hiyo alianza kuwatuhumu watendaji wa wizara hiyo kuendesha mradi huo mwendo wa kusuasua kinyume na maelekezo ya mradi mzima.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema mradi huo uliotakiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2008 ndani ya miaka miwili, mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
  Ndugulile alisema badala yake wizara imezuia watu kuendeleza makazi yao kwa kipindi chote hicho na hakuna jibu sahihi linalotolewa la kuanza rasmi kwa mradi huo.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema endapo maofisa hao walikuja hapo kutoa maelezo tu na sio kutoa muda kamili wa kuanza kwa mradi basi watambue hakuna kitu kitakachofanyika.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Tumechoka na maelezo yenu, kila siku tuna mipango hii na ile, leo hapa bila ya kutueleza lini mji mpya utaanza, wapi mtaanzia na lini fidia zinaanza kulipwa, hatutawaelewa patachimbika hapa," alisema Dungulile huku akionekana kukerwa na jambo hilo.

  [/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]Katika hali inayoonyesha kuwa baadhi ya viongozi wa Kisiasa hasa madiwani na Mbunge wa Kigamboni wanataka kugeuza huu mradi kuwa mtaji wa kisiasa soma hapa chini kauli zao.
  Maofisa Ardhi watimuliwa kikaoni[/FONT]

  [FONT=&quot]Alisema sasa madiwani wote wamechoshwa na hali hiyo na aliomba kama maofisa hao wamekuja hapo hawana majibu sahihi ya maswali yao basi warudi walipotoka wakatafute majibu au wakakutane na wanaharakati hao waendeshe mradi huo hewa.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Leo tunashangaa mnakuja hapa kuongea na sisi madiwani, lakini tunafahamu kuna kikundi kimoja cha watu mnakutana nao na kujadiliana nao juu ya mradi huu, sisi kama madiwani na wabunge hatujui chochote, hii ni ajenda mbaya dhidi ya CCM. Hatupo tayari kuona mnaichimbia kaburi CCM na sisi wenyewe tunaona," alisema Diwani Msawa.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]


  [/QUOTE] [FONT=&quot]Hata hivyo, diwani Anderson Chale wa Kata ya Kijichi alionekana kushangazwa na watendaji hao kuitisha kikao bila kujiandaa na badala yake wanaonyesha umahiri mkubwa wa kisiasa badala ya kazi ya utendaji waliombea ajira.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema wananchi wa Temeke wamechoshwa na miradi isiyo endelevu inayofanywa na wizara hiyo kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo. Alimuomba Meya wa Manispaa hiyo, Maabad Hoja, aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao kuahirisha kikao hicho mara moja kwa sababu imeonekana maofisa hao hawakuwa na jipya.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kauli hiyo iliungwa na Mbunge Mariam Kisangi, ambaye alifananisha mradi huo sawa na bomu linalotaka kulipuka, ambapo alionya kama hakutachukuliwa hatua ya haraka yatatokea mapigano kama yanayotokea migodini kutokana na wananchi kuishiwa na subira.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema mradi huo ulipoanza wananchi wengi waliupokea kwa mikono miwli wakitarajia kupata matumaini mapya, lakini matumaini hayo yameanza kupotea kutokana na mradi huo kutoanza kama walivyoelezwa kitu ambacho wengi wao sasa wameanza kuichukia serikali yao.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]"Mimi ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, najua mambo yanayotokea kule lakini nahisi na Temeke [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]tutashuhudia kwa sababu watu wamepoteza subira na matumaini, nyie watendaji mnawasha moto kwa uzembe wenu, tunataka haya yasitokee fanyeni kazi kwa uaminifu mkubwa," alisema Kisangi.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alisema kimsingi wanatemeke rasilimali yao kubwa wanayotegemea ni ardhi, ikiwa ardhi hiyo inachukuliwa kiujanjaujanja hawatakubali na ndipo watakapoamua kuitetea kwa nguvu zao zote.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, maofisa hao akiwemo mratibu wa mradi huo Majura hawakuweza kutoa majibu hayo, kitu kilichosababisha Meya wa Manispaa hiyo kuvunja kikao hicho na kuwaagiza maofisa hao kwenda kutafuta majibu hayo na kuyawasilisha tena kwa viongozi hao kabla ya kazi ya kuhamasisha wananchi haijaanza.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]SOURCE: NIPASHE [/FONT]
   
 18. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Lazima madiwani watafute kila nnjia ya kuahirisha vikao ili idadi ya vikao iongezeke na posho iongezeke pia
   
 19. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ishu inakwendaje? any updates
   
 20. che-guavara

  che-guavara Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Isije ikawa mambo ya airport wananchi wanaamishwa baada ya miaka 30 fidia ya zamani.WANANCHI harakisheni kupitia kura zenu 2015.la sivyo mtauzwa mpaka wenyewe.
   
Loading...