nyani jike
Senior Member
- Feb 23, 2016
- 176
- 223
Kigamboni ferry pameoza ufisani na rushwa ndogondogo za hali ya juu,tatizo sio panton tu na uongozi mzima wa TAMESA,Askari Wa suma jkt,jeshi la police,pamegezwa pango la kupatia vijisenti,unakaa kwenye foleni masaa 6 na foleni ipo soko la samaki ferry,hivi kila mtu kigamboni ni anakibali maalum cha kupita no entry??kuna rushwa za elfu 5,10,2.wanazopokea wasimamizi Wa kivuko kila MTU pale anamamlaka yake,nashindwa kuelewa kivuko ni sehemu ya mtaji Wa watu au ajira?maaskari punguzeni wizi na tamaa za kijinga ferry tumechoka wananchi fanyeni kazi,sijaona msaada Wa hata Mmbunge Ndugulile kwenye hili swala wala sijui kazi zake nini tokea kawa mbunge yeye ni kuzungumzia tu habari za mashamba na makazi,kama hilo ndo Kero tu kwa wananchi?rais magufuli safisha upya uongozi wa ferry wafukuze kazi wafanyakazi wote Wa kivuko kama kweli unatumbua majipu haiwezekani ukae hapo magogoni usijue kero za hapa ferry.