Kigamboni bridge; mbona bei zinachanganya?

Nyanidume

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
2,381
1,073
Amani iwe kwenu wakuu! Siku ya kwanza kupita daraja hilo nililipa tsh 7000 kwa maelezo kwamba gari kuanzia tani 2-7 hiyo ndiyo bei yake, mimi nilikuwa na kenta tani 2. Nikapewa risiti isiyokuwa na nembo ya TRA, iliniuma sana kwani sikufikiria kama ningekuta bei kubwa kiasi hicho na mbaya zaidi nilikuwa nimeshatoa tsh 2000 kwa trafiki baada ya kunikamata na kunitishia kuniandikia.

Sasa leo kuna jamaa yangu kapita na gari hiyohiyo yeye kachajiwa tsh 2000 na akapewa risiti yenye nembo ya TRA!!! Naomba mwenye ufahamu wa hili swala atoe il-mu hapa maana nahisi nitakuwa ‘nimepigwa’.
 
Hata mimi leo nimepita na gari ya carry tani 2 kutoka k/koo kuja kibada na nilikuwa nimebeba kamzigo nyuma ,tumechajiwa 2000 tu kwenda na kurudi 2000 jumla 4000...
 
Back
Top Bottom