Kigali Mbali . . . Kigali Mbaaali Tukumbukane . . .

Dominique+2.JPG
 
Kuhusu hao wadada sitasema chochote, isipokuwa nakumbuka mambo mengi mazuri niliyoyaona nilipoenda mwaka jana. Tofauti na Superman aliyepanda ndege, mimi nilienda kwa njia ya barabara na nilifurahia sana! Utamu unaanzia pale boda, Rusumo. Baada ya kuvuka daraja na kufika upande wa pili wa boda unakabidhiwa mfuko wa karatasi ambao utawekea vitu vyako na unaacha ile mifuko yetu ya rambo (plastiki) pale. Inasemekana kukutwa na mfuko wa rambo/plastiki ndani ya Rwanda (sijui sehemu zingine, maana mimi nilienda Kigali) ni kama umekutwa na furushi la bangi!! Baada ya hapo ni mashamba ya ndizi (migomba), hadi unakaribia Kigali. Ni mandhari inayopendeza sana, sijafika Bukoba (Kagera) lakini wanafananisha na mandhari ya huko! Kumbuka wao wana Right Hand Driving, hivyo unaweza kubabaika kidogo, maana unaona kama unaendesha wrong site!
Ukifika mjini ndo usiseme, ni kusafi hakuna mfano, mitaro, barabara, madukani, sokoni, nk. ni baaaaaaaab kubwa wajameni. Ni kweli ni wakarimu, hasa wakijua wewe ni mTZ. Nilifika maeneo ya makumbusho ya yale mauaji ya kimbari! Hilo sitaki kulisimulia, ila kuna siku nitaweka zile picha za mafuvu na mifupa (leo naogopa kuziweka msije mkanipiga bure, hasa ukilinganisha hao wadada na baada ya kufa watafananaje, joke)!
 
sio Afrika mashariki tu ,wakikubali kubinafisisha ni bora hata serikali yetu ibinafisishwe tu hata kwa miaka 20, labda tutajipanga zaidi na kujua wapi tuankotakiwa kwenda, maana kwa sasa serikali inajiendea tu bila kichwa wala miguu..
Nitajisikia vema sana kumpigia kura kagame kuwa Rais wangu wa Afrika Mashariki . . .
 
Back
Top Bottom