Kigali Mbali . . . Kigali Mbaaali Tukumbukane . . .

He! kumbe superman ni binti. Maana anasema tumeenda na kurudi salama halafu picha zilizofuata ni binti tupu.
 
Mmmh rwanda ni warembo kama hujazoea kuwaona lakini wabongo wako poa zaidi nimekaa rwanda na uganda miaka kadhaa nimeinteract sana na waganda n westerners kule Uganda yaani wanyankore na wahima ambao wengi ni asili moja na wanyarwanda wengi kwa muonekano wa nje ni safiiii ila kuna baadhi ya vitu hawawezi .....kama wakibongo ambao wako full kuanzia muonekano hadi michakato ya ndani ya nyumba.....
 
Good question Mkuu.

Niliyoyaona na kuyasikia:

1. Kila mwananchi anatakiwa akubali na kukiri kuwa kulikuwa na Genocide na kuwa kulikataa hili ni kosa kisheria. Msingi wake ni kumfanya kila mtu akumbuke walikotoka na kuepuka kutokea madhara kama yale. Hilo pia linawafanya wawe na mshikamano wa kuijenga nchi yao.

2. Nilifika usiku, nilishangaa kuona usiku kulikuwa na White guys wanaranda randa mitaani na wazawa tena kwa furaha tu. Hii ni majira ya saa nne na kuendelea. lakini pia niliona police na JWTZ wa kule wakilinda mji/mitaa very strategically. Jamani Kigali ni shwari. Ingekuwa TZ nina uhakika mtu angepigwa roba.

3. Kuna mtu alisahau au kundondosha miwani ya bei mbaya Airport. Nimeshuhudia mdau akifanya jitihada ya kuifikisha security kuwa ameiokota. Ingekuwa bongo sijui ingekuwa vipi.

4. Watoto wa kike wako wengi katika nyanja ya Jeshini na Police na Security. Kazi ni kazi hakuna mchezo. Sasa na uzuri wao ni balaa. Askari wa kike aliniomba nifungue bag langu la laptop akague Airport, du, ilikuwa ni neema tu.

5. Barabara zinajengwa mjini na nyingi ni nzuri. Lami almost kila mahali na mji ni msafi. Taa za barabarani kila mahali. Traffic laws zinafwatwa sana. Hakuna msongamano wa mahari kama Nairobi, Kampala au DSM.

6. Nimeambiwa Kagame kila mwanzo wa mwaka anakuwa na makubaliano binafsi na appointee wake wote huku kila moja akiwa na targets zake binafsi. Mwishoni mwa mwaka kuna assesment. Kama performance yako ikiwa below standard anakutoa. Kwa hiyo watu wanafanya kazi.

7. Corruption at your own risk. Jamaa akisikia umetuhumiwa kwa rushwa, kwanza anakutoa katika cheo chako kisha unafanyiwa uchunguzi. Ukibainika ni majungu, unapewa promotion. Kama ni kweli, imekula kwako unaenda mahakamani.

8. Utawala wa sheria kama kawa, nilijaribu kuingia na za kichina china kama za bongo katika mambo fulani ili kupima kama jamaa wata-bend, lakili nilipiga hola.

9. majengo mapya ni mazuri na construction inaendelea.

10. Sehemy yao kama ya Kariakoo wanaiita "Commercialle", ina mitaa ya biashara mingi lakini well organized na misafi.

And many more. Watanzania tuna mengi ya kujifunza.
Mkuu wetu wa kaya ameshindwa kabisa kwenye namba 7.
 
Already missing Kigali . . .

Mji Mzuriiiiiiiiiiiiii . . . Msafiiiiiiiiiiiiiii . . . Very Organized! I wish . .

tuwekee na picha ya mji. naona umetujazia wadada tu. warembo hawaishi Superman kila siku wanazaliwa wapya.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom