GE2025 Kigaila: Hakuna mkono wa serikali CHAUMMA

GE2025 Kigaila: Hakuna mkono wa serikali CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,450
Reaction score
5,276
"Siku hizi wanaruka na helkopta, inaonekana ile Helkopta wamepewa na serikali. Sisi tunaoruka na helkopta CHAUMMA leo ndiyo tulikuwa tunaruka na Helkopta Chadema mwaka jana, mwaka juzi mpaka mwaka 2005. Leo wao wanaruka na Helkopta? sasa wakubali kama hii Helkopta tumepewa na serikali waseme ya Chadema ya miaka hiyo ikiwemo ya 2020 ambayo Lissu alikuwa anaruka nayo wasema kuwa ilikuwa ya CCM.

Sisi hatujahama Chadema, tumehama na Chadema, tumeacha darasa kule na wale jamaa wanne ambao wote kwa pamoja hawajawahi kutafuta Helkopta, hawajui inapopatikana, hawajui gharama yake na hawajui namna gani inavyofuatiliwa.Mmeona gari hapa imeondoka, inaenda Tanga kwaajili ya kusambaza mafuta kwasababu tunajua nchi hii viwanja vya ndege vyenye mafuta ni vichache na hatujawahi kukwama hata siku moja na tangu 2005 tunafanya."-Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA akizungumza na wanachama wa Chama hicho kwenye ziara ya kikazi Mkoani Njombe.

 
Back
Top Bottom