Kifo cha upinzani baada ya Uchaguzi

Kifo cha upinzani baada ya Uchaguzi

Ni ukweli usiopingika kuwa Chadema ni chama kilichoisumbua sana ccm,chama tawala toka vyama vingi viliporudishwa mwaka 1992.

Mwalimu nyerere aliwahi kutuasa kuwa Chadema inaweza kuwa chama pekee cha upinzani kitakacholeta upinzani wa kweli kwa ccm.

Ni bahati mbaya sana kwa Chadema kushindwa kusimamia ajenda yake ya muda mrefu...kuhusu ufisadi.

Chadema imepoteza mwishoni mwa mapambano baada ya kujizika kwenye kaburi la kuutetea ufisadi kwa kujaribu kumsafisha Fisadi.

Kwa kuwa wananchi walishahamasika kuupinga ufisadi na mafisadi basi wanasiasa hawana budi kutambua kuwa ufisadi ni kete ya kuwaangusha au kuwapitisha katika uchaguzi huu.

Uchaguzi huu hautambeba mtu kwa jina la chama zaidi utambeba kwa jitihada zake kama yeye.

Baada ya uchaguzi huu Chadema itapumzishwa rasmi kwani imeonekana kuwa ni sehemu ya genge la wasanii wa kisiasa hasa baada ya kuwakumbatia mafisadi au watuhumiwa wa ufisadi.

Baada ya wananchi hasa wenye mrengo wa kipinzani kupiga kura zao kwa hasira..tutahitaji kuujenga upinzani wa kweli....upinzani wenye sera kinzani na ccm.

Hili litakuwa ni jukumu la watanzania wote wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli na endelevu!

Jambo hili halitawezekana mpaka pale wana mabadiliko wenye nia ya dhati watakapoanzisha chama kipya cha upinzani chenye mrengo kinzani bila unafiki dhidi ya ccm.

Haya ni maoni ya Jingalao.

hupendi acha!


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom