FATHER OF HISTORY
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 802
- 468
Kama ndiyo ma RPC Wenyewe ni hivi,tunasafari ndefu ya kwenda,hivi kama mtu amekiuka sheria ndiyo adhabu yake kuuawa na bomu?.Hivi kama RPC anakaribia kustaafu ndiyo aamuru kuua watu? Kazi ya wanahabari ni kuandika habari,sasa yule mwandishi aliuawa kwa lipi? je ,RPC alikijua alichotaka kuandika yule mwandishi?,ni sheria gani ambayo mwandishi alikiuka? kwani polisi hawa wezi kuzuia vurugu mpaka wa ue?picha zinaonesha polisi akimfyatulia bomu yule mwandishi,je adhabu yule mwandishi ndiye aliye vunja sheria au kile kikundi chote kilichokuwa pale? kama ni yeye peke yake,je umati ule wote wa polisi ulishindwa kumkamata mtu mmoja nakumpeleka kituoni? kama ni wengi waliokuwa pale,kwanini adhabu hii ya kifo impate maskini huyu mwandishi na wengine kuachwa kama adhabu hiyo ni stahiki kwa wavunja amri? RPC na jeshi la polisi lijitathmini upya,watu wakichoka wataanza kushughulika na mtu binafsi badala ya polisi kama taasisi,maana polisi wenyewe tunao huku huku mtaani katika nyumba za kupanga,sjui itakuwaje,nawapongeza wale police waadilifu na wale wenye kutii amri ya kuua kama vile kazi ya polisi ni maisha ya peponi ole wao. Labda ni upeo wangu wa kuelewa mambo ni mdogo,lakini naona hapa kunatatizo
Police wengi wanavuta bangi, unategemea nini kuhusu usalama wa raia? Jeshi la police limejaa wavuta bangi! Ni polisi wachache sana wanaofanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi yao, wengi utawaona walivyo na hasira na raia hata kama mtu hana kosa/hatia yeyote. Pamoja na hayo, kulikuwa na fujo gani hadi kuamua kutumia nguvu kiasi hicho? Tufike mahali tuanze kuhoji matumizi ya siraha kama mabomu ni nani anagharamia? Tufahamu nani ni nani, amefikaje hapo alipo?