HadithiZaRuvulyDeFinisher
Member
- Jul 14, 2022
- 7
- 12
Na : ATHUMANI RUVULY
Binti mmoja ambaye alitokea katika Familia ya kimasikini sana, alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akaishi katika nyumba nzuri na ya kifahari sana .
Pamoja na maisha mazuri lakini binti huyo alifumba mambo na kufumbua upya, kitendo hicho kilimfanya apuuze sehemu alikotoka na kujibatiza kuwa yeye ni mzaliwa wa mjini na sio mzaliwa wa Kijijini kwao tena, Pamoja na mabadiriko hayo bado Mungu alimpa kumbukumbu kwani alikua akituma pesa kidogo kidogo nyumbani kwao japo hakuhitaji kabisa kwenda kijijini kwao na kujikuta anasahau tabu za maisha yake yote ya mateso aliyopitia kijijini kwao .
Katika maisha yake ya mjini Binti huyo alijitambulisha kwa marafiki zake kwamba yeye ni Mzaliwa wa Dar es salaam huku akidanganya kuwa Wazazi wake wamefariki na yeye alikua Mtoto pekee katika familia ya kitajiri sana hapo mjini na Wazazi wake walipofariki walimuachia mali nyingi sana, Binti huyo alivaa uhusika huo kwa sababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri nae hakuhitaji kudhalilika mbele yao .
Baada ya kuishi huko Kwa muda mrefu bila kuwasiliana na familia yake na pasipo kufika Kijijini kwao, Wazazi wake walipata wasiwasi mkubwa sana, Fikra zilifika mbali hali ambayo iliwapelekea kufikiri kuwa huenda Binti yao huko alipo atakuwa kapatwa na matatizo. Wazazi wakiwa na wasiwasi huo ilibidi familia wachange nauli na ikamlazimu Mama mzazi wa binti huyo kupanda gari akiwa na Jirani ambaye alibahatika kufahamu sehemu aliyokuwa anaishi Binti yule .
Baada ya Safari ndefu Mama alifika salama na Kwa uwezo wa Mungu, Mama alimkuta Binti yake akiwa na afya njema, Binti hakuwa na tatizo lolote, Kitendo hicho kilimkasirisha sana Binti yule kwa kumuona Mama amemfuata mjini pasipo taarifa yeyote, Hakika binti alikasirika mno .
Binti yule hakumsalimia vizuri Mama yake na muda wote alikua akimlaumu Mama yake kwa kusema :
" Kwanini hakupiga simu kwanza Mama kabla hujachukua hatua ya kunifuata huku nilipo ? Kwa sasa hali yako sio nzuri na umri umekutupa mkono Mama na kama ulikuwa unashida na Pesa ungeniambia nikakutumia lakini sio kama ulivyofanya tatizo nini Mama ?
Mama akiwa anatokwa na machozi ya furaha usoni amejawa na tabasamu bashasha alimjibu Binti yake :
" Shida yangu haikuwa Pesa bali nilitamani sana kukuona binti yangu , Nisamehe kama nimekosea kuja hapa nyumbani kwako na usijali sitoishi sana hapa nafikiri nitaondoka mapema sana kwa sababu nilitamani kukuona tu nimekukumbuka binti yangu kipenzi sijakuona muda mrefu .
Pamoja na upendo huo alio uonyesha Mama huyo bado Binti hakuhitaji kuishi na Mama yake hivyo alimdanganya Mama yake Kwa kumwambia kwamba nyumba anayoishi sio yake bali ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na sheria ya kazi aliokuwa anaifanya, hivyo Mama yake hakuwa na nafasi ya kuishi ndani ya jumba la binti yake .
Mama hakuwa na maneno wala kinyongo alimsogelea Binti yake akamgusa shavu na kumwambia : Hata usijali binti yangu, shida yangu ilikuwa kukuona tu na sio kuishi hapa kwako na kwakua nimeshakuona hapa nafsi yangu imetulia hivyo muda wowote narudi kijiji kwetu usijali mwanangu .
Binti alimuacha Mama yake apumzike siku ile na siku iliyofuata kwa malengo siku ya tatu Mama apande gari na kurudi Kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda kufurahia, Marafiki hao walipofika Walimkuta Mama wa Binti yule akiwa nje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwafuata Marafiki zake haraka haraka ili Mama yake asijitambulishe kwao, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke mapema.
Walipotaka kujua Mama waliomkuta ni nani yake , Binti yule alijikuta anadanganya kwa kusema : Huyo Mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta Mtoto wake akakosea nyumba hivyo ikabidi nimsaidie si unajua tena Marafiki zangu msaada ni popote, msaidie yeyote hatakama humfahamu, na bahati nzuri namba za simu za mtoto wake alikuwa nazo kwahiyo nimeshampigia mwane ninaamini atakuja kumchukua muda wowote, Binti yule aliongea maneno hayo akiamini kuwa kesho yake anamuondoa Mama yake pale nyumbani kwake hivyo rafiki zake hawatamuona tena .
Wakati Binti yule akiongea maneno hayo hakujua kuwa Mama yake anasikia kila alichozungumza, baadae Binti alistuka alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aondoke na marafiki zake kumuona Mama yake akitokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumuona akaingia kwenye gari na kuondoka na marafiki zake .
Baada ya mizunguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta Mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui Mama alipokwenda kwani nae alijua wameondoka pamoja .
Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa manane lakini Mama yake hakurejea, Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kilimuuma sana , Hofu iliyoambana na wasiwasi mkubwa iliutawala mwili wa Binti yule , hapo ndipo alianza kukumbuka maisha ya shida waliyopitia yeye na Mama yake na jinsi Mama alivyoteseka kwa ajili yake .
Machozi yalinza kumtoka Binti yule akijutia kwa mambo aliyomfanyia Mama yake, Binti alimtafuta Jirani aliyemleta Mama yake lakini nae hakuwa akifahamu chochote kuhusu Mama yule, Usiku ulipita Binti akiwa macho, yalipofika majira ya asubuhi na mapema alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao na wafanyakazi wenzake .
Baada ya masaa kadhaa Binti alishindwa kuvumilia, alikwenda kituo cha Polisi na kuanza kumtafuta Mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye ya pili ikapita bila kumuona Mama yake, Wasiwasi ulizidi moyoni mwa binti yule .
Baada ya masaa kadhaa kupita katika siku hiyo Bibti alikuwa ofisini ameikaa hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja kumtembelea ofisini kwakwe, walianza kuongea akiwa hana raha wala amani, Rafiki yake alipomuuliza tatizo linalomsumbua ? Binti alipotaka kumueleza rafiki yake ukweli kuhusu Mama waliomkuta siku zilizopita nyumbani kwake, Rafiki huyo alisema : Halafu shoga yangu nilitaka kusahau, unamkumbuka yule Mama ambaye tulimkuta kwako juzi juzi hapa ukatuambia kwamba kapotea akiwa anamtafuta Mama yake ?
Binti yule aliposikia hivyo alistuka na kuuliza haraka haraka : Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?
Binti alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua rafiki yake kamuona wapi Mama yake .
Rafiki alijibu : Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu moja kule mapanda njia kama unakwenda bank, nimekuta watu wengi wamezunguka eneo lile niliposogea karibu kujua tatizo ni nini, Duuuh nilishangaa kumuona yule Mama kumbe kagongwa na bodaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi na mimi nikapita kama sikuona chochote mwenzangu si unajua kesi tena, Sasa baadaye narudi nikapita njia ile ile Masikini kumbe watu walimuacha Mama wa watu pale pale mpaka Polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi Bibi wawatu kashafariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia .
Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu, alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake .
Binti alipoulizwa sababu za kupatwa na hali hiyo, ndipo alipoamua kuwaelezea ukweli wote, kila mtu alimshangaa kwa kumficha Mama yake, walihangaika kuutafuta mwili wa rafiki yao wakakuta maiti ya Mama yake ikiwa hospital, Marafiki zake walimsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini kwao.
Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wa Binti yule hakuhitaji kuendelea nae tena hivyo alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tukio hilo, Binti alishikwa na msongo wa mawazo, hali iliyopelekea kuwa mtu wa kulia kila siku ilikua mtu wa kulia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, jambo lililopelekea afukuzwe kazi na kunyanganywa Jumba la kifahari alilokuwa akiishi kwa sababu ilikuwa nyumba ya Kampuni, Binti akaishia kuwa mtu wa mtaani, analala kwa marafiki zake na kila siku yupo mtaani akitafuta ajira, Marafiki waliokuwa wanampatia hifadhi walimchoka na kumfukuza Binti akarudi Kijijini kwako akiwa hana mwelekeo wowote .
Kutokana na mawazo mazito aliyokuwa nayo Binti aliamua kujiua mbele ya kaburi la Mama yake.
Kama kisa hiki kimekugusa na unampenda sana Mama yako, Pia unakumbuka asili yako #SHARE kwa wingi Chapisho hili kwa Marafiki zako na sehemu mbalimbali, Kuna MTU atajifunza kitu kupitia wewe ahsanteni
Hakikisha umeni Follow ili usipitwe na Mikasa, Riwaya na Hadithi mbalimbali zinazokuja .