Kifo cha CCM kimetimia

Raha ya ndoto,iote usiku,ndoto za mchana utaambulia maruhani na maluweluwe.

Tatizo lene PolCCM mna akili za kupe. Ng'ombe anachinjwa, kupe hana habari, ng'ombe anachunwa, kupe hana habari, ngozi inawambwa, kupe hana habari.... ngozi ikianza kukauka ndo anastuka na inakuwa tooooo lateeee!
 
mhhhheeee. Tusubiri tuone, JK kasema hayuko tayari kukabidhi nchi kwa yeyote isipokuwa ccm, hapo napo vipi? anajua anajeshi la serikali lisilo la wananchi- mtakula mkong'oto nyie mpakaaaaaa- labda tuwe wakomavu kama Misri na Libya, tupo tayari?
 
Nawe, usiwe mbaguzi mh.Mizengo Pinda wa kupindisha issue, ambaye pia ni mwongo (kwa mujibu wa G.Lema) mbona hayumo kwenye orodha yako.

Pia, usisahau polCCM kuanzia igp hadi akina kamhanda wote wa mikoa na wilaya.

Pinda ana ulimi wenye sumu, unaweza mchukia sasa, ukimpa nafasi ya kujieleza anakuwa rafiki yako. kumbuka, Ni Pinda huyuhuyu aliyemaliza mgogoro wa Mtwara juzi, laikini pia, serikali humtumia mahala pale ambapo wamekwisha angukia pua na mara nyingi anafanikiwa.
 
Nawe, usiwe mbaguzi mh.Mizengo Pinda wa kupindisha issue, ambaye pia ni mwongo (kwa mujibu wa G.Lema) mbona hayumo kwenye orodha yako.

Pia, usisahau polCCM kuanzia igp hadi akina kamhanda wote wa mikoa na wilaya.

Hivi yule DCI bado anapumua?
 

Ni Waziri mkuu dhaifu kuliko wote ambao Tanzania imepata kuwa nao...
 
Mimi nawapenda JK, Mangula, Kinana, Makamba na wenzake wote wanasaidia Kuiua CCM. Kumbuka kauli za Makamba wakati ule zilileta mgongano ndani ya CCM na hata alipo ondolewa aliwambia kuwa anakwenda kuwandalia makao!!!
Sasa inaonyesha wewe hupendi CCM ife kwa sababu either ni mshauli wa siri ama unanufaika nayo!!
Nakushauri uwapende watu wote wanaoiua CCM akiwemo JK ili upinzani ushike madaraka!!!
 
Badala ya kuandika kuelewesha watanzania juu ya dhana iliyopo kwa Chama chako ni cha kidini(kikatoliki) na kikanda na ukabila(ukaskazini na uchaga),ambapo hadi leo viongozi wa Chadema wameshindwa kukanusha tuhuma hizi wewe unapoteza muda kwa kuleta ngonjera zisizo eleweka juu ya CCM! Mpuuuuuzi hana fikra siku zote!
 
CCM isipokufa 2015 basi hakitakufa tena kabisa.
LAZIMA KIFE 2015. Kuanzia November 1, 2016 CHAMA CHA MAJAMBAZI KITABAKI HISTORIA NA KUNA WATU WENGI SANA WATAKAOHAMA NCHI HII AKIWEMO WASIRA, LOWASSA, NCHEMBA, KINANA, NAPE, MKAPA na wengine wengi tu.
 
Hata mpumbavu shibuda, alishalonga kuwa ccm itafia mikononi mwa kikwete na kikwete atahakikisha ccm inakufa na kuizika. R.i.p ccm
 
Mnaongelea kuhusu hao Mawakala wa kifo cha ccm?
JK hakika ameisogeza pakubwa sana serikali yake kuelekea kaburini...tunampongeza.

Majuzi nikiwa ofisini kwangu nikaambiwa kuna ugeni. Ghafka nashangaa wameingia watu na makamera makubwa, wanajieleza kuwa wamefika ili kuja kuelezwa mafanikio yoyote ya awamu ya 4 yaliyotokea katika eneo la ofisi yangu...hakyanani nilibadilika sura hadi waligundua.

Hakika ilinichukua kama dakika 15 kupata muafaka na uongozi wa kichwa changu ili kuwapa wanachotaka...!
Huku ndiyo kukosa uhalali alikokusema Nyerere, ambapo sasa serikali ya J K inatumia mabavu kupata uhalali.
My hairs!
 
ebu tufafanulie wewe huo ukanda, ukabila na udini, ina maana zitto ni mkristo(rc) na mchaga?. Je said arfi?. Kweli watz kama wewe ni mburula wa uelewa!
 
CCM isipokufa 2015 basi hakitakufa tena kabisa.
LAZIMA KIFE 2015. Kuanzia November 1, 2016 CHAMA CHA MAJAMBAZI KITABAKI HISTORIA NA KUNA WATU WENGI SANA WATAKAOHAMA NCHI HII AKIWEMO WASIRA, LOWASSA, NCHEMBA, KINANA, NAPE, MKAPA na wengine wengi tu.
ebu nifafanulie maana ya kufa kwa chama mkuu, mimi nadhani ccm mwaka 2015 kitakuwa cha upinzani, na si vinginevyo!
 
aliyekudanganya mgogoro wa mtwara umekwisha ni nani?
amesema huwenda walioharibiwa mali zao ktk mgogoro wa gesi juzi wakafidiwa

sasa tandahimba wanasubiri hao walioahidiwa kulipwa, walipwe ili nao wapachimbe,
unakumbuka nao hadi leo hawajafidiwa baada ya maduka, nyumba na magari yao kuchomwa moto na polisi wa ccm? ktk vurugu za mwaka jana
sasa pinda kaenda kumdanganya bosi wake kwamba mgogoro umekwisha.
RIP magamba
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…