Jumanho
Member
- Sep 14, 2010
- 37
- 5
Inakaribia miaka 30 sasa tangu Tanzania ishiriki mara ya mwisho kwenye mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika, CAN. Na kwa hali jinsi ilivyo kwasasa sidhani kama tunaweza kushiriki kwenye mashindano hayo milele. Mimi nadhani ni kutokana na mfumo wa soka letu na haswa klabu kongwe za simba na yanga ndio zinadumaza maendeleo ya mchezo huu hapa nchini. Kwa mtazamo wangu ili soka la Tanzania liendelee inabidi hivi vilabu kongwe vibadilike au vife kabisa kama zilivyokufa klabu kongwe za majirani zetu kenya na Uganda. Hii itasaidia sana TFF kufanyakazi bila kuwa na upendeleo kwa timu yoyote.
Wewe mdau mwenzangu unaona nini kifanyike kuinua soka la Tanzania?
Wewe mdau mwenzangu unaona nini kifanyike kuinua soka la Tanzania?