Kifanyike nini kusaidia kuinua Soka la Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifanyike nini kusaidia kuinua Soka la Tanzania

Discussion in 'Sports' started by Jumanho, Sep 15, 2011.

 1. Jumanho

  Jumanho Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inakaribia miaka 30 sasa tangu Tanzania ishiriki mara ya mwisho kwenye mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika, CAN. Na kwa hali jinsi ilivyo kwasasa sidhani kama tunaweza kushiriki kwenye mashindano hayo milele. Mimi nadhani ni kutokana na mfumo wa soka letu na haswa klabu kongwe za simba na yanga ndio zinadumaza maendeleo ya mchezo huu hapa nchini. Kwa mtazamo wangu ili soka la Tanzania liendelee inabidi hivi vilabu kongwe vibadilike au vife kabisa kama zilivyokufa klabu kongwe za majirani zetu kenya na Uganda. Hii itasaidia sana TFF kufanyakazi bila kuwa na upendeleo kwa timu yoyote.
  Wewe mdau mwenzangu unaona nini kifanyike kuinua soka la Tanzania?
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  kumbe jibu (in red) unalo alafu unatuuliza japo yaweza lisiwe sahihi! Nadhani ungetoa utaratibu gani utumike kuziua ili tuanze utekelezaji.
  Lakini cha msingi ukumbuke miaka kama 15 hivi iliyopita wakati mheshimiwa sana Muhidini Ngolanga amejimilikisha FAT (TFF), Ndugu Jenerali Ulimwengu aliliona tatizo la mpira (na michezo kiujumla) wa Tanzania na akatoa wazo la kusaidia kutatua hilo tatizo. Alipendekeza (kutokana na hali ya wakati huo) tujito katika mashindano ili tujipange ili tukija kurejea tuwe 'binadamu'nasi kama wengine ...muulize jirani yako au yeyote anayekumbuka huo uamuzi ulipokelewaje!!??
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Naungana na fikra zako, hizi klabu 2 ndio mchawi mkubwa wa soka la tanzania, na kama zitaendelea kuwa na nguvu, hakika hata miaka 15 ijayo sitarajii makubwa katika soka la bongo, tutaendelea kujipa ushabiki kwa timu za majuu tu, kwani huko ndio wapenda soka wanakopata faraja
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jibu la swali hili ni pana sana lakini kwa ufupi, naamini ukua tunatakiwa kuanza upya. Katika mikakati mipya tutakayojipangia, maendeleo ya soka iwe ni sehemu ya mipango ya kitaifa ya maendeleo. Watoto wanaoonekana kuwa na vipaji vya michezo (si mpira tu) waendelewe kulingana na vipaji vyao. Huu mtindo wa kuja kuokota wachezaji waliojikomaza wenyewe hautatufikisha popote, wachezaji wanatengenezwa.
  Kuna wakati tuliahidiwa (wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nadhani) kuwa kutakuwa na mjadala wa kitaifa kuhusiana na suala hili, sijui huo mjadala umeishia wapi. Naamini
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hapo umeshamaliza ila kikubwa zaidi ni sisi wenyewe kukubali mabadiliko na sio kuichia tu serikali yenyewe.
   
 6. Jumanho

  Jumanho Member

  #6
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapo kwenye red, chakufanya wale wenye uwezo wa kumiliki vilabu kama alivyofanya Bakharesa (Azam FC) wafanye hivyo na kuviendeleza kama ambavyo wanavyofanya Azam. Hii itasababisha natural death kwa Simba na Yanga. Vilevile pia management ya hizo timu isiwe chini ya Watanzania kwa kuwa ninaamini na nina uhakika kuwa hakuna mtanzania ambaye si simba au yanga, kwa hiyo unapofanya management yako kuwa ya watanzania italeta usimba na uyanga halafu utakuwa kama unatwanga maji kwenye kinu. Hiki ndicho walichofanya wenzetu wa kenya na uganda na ndio maana sasa husikii siju Gor Mahia, SC Villa au Express bali unasikia Bunamwaya, Sofapaka etc. Kwa taarifa tu, Hatuwezi kuwa na timu bora ya taifa wakati vilabu vyetu na hata ligi kuu yetu si bora
   
Loading...