Kidato cha nne kupiga ‘pepa’ kesho

Kidato cha nne kupiga ‘pepa’ kesho

drclark

Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
57
Reaction score
12
Jumla ya watahiniwa 408,442 wa kidato cha nne wanatarajia kuanza mitihani ya kidato cha nne itakayoanza kesho, ikiwa ni idadi pungufu ya waliofanya mtihani huo mwaka jana.

Akizungumza na wanahabari leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dk Charles Msonde amesema mwaka jana kulikuwa na watahiniwa 448,382 waliofanya mitihani huo.

Dk Msonde amesema maandalizi yote ya mitihani hiyo itakayomalizika Novemba 18, mwaka huu yameshakamilika.

Amewataka wanafunzi, walimu na wasimamizi kujiepusha na udanganyifu wa mitihani kwani baraza hilo halitasita kuchukua hatua za kisheria, ikiwamo kuwafutia matokeo.
 
madogo mtakao piga pepa kesho mkifaulu kwenda advance hakikisheni hamuendi private mtakuja kulia ,mtakosa mkopo
 
Mdogo wangu anafanya mtihani mwaka huu kuanzia kesho, namtakia yeye na watahiniwa wenzake wote mtihani mwema!

Kaka ...
 
Nawatakia mtihani mwema wote, na mwanangu Angel nawatakia kila lakheri Mungu awafanye muwe vichwa na msiwe mkia. Katika jina kuu Yesu Amen.
 
form 4 wote mtihani mwema Tuzidi kuwaombea wote waepukane na Magonjwa na hofu za Mitihani.

Mwenyezi Mungu awajalie Afya tele na Roho Mtakatifu awatangulie kwa kila watakachoenda kuandika kiwe cha ukweli.
 
Kesho ndio tamati yenu ya kupokea elimu bure. Msiseme hatukuwaambia.

Mkimaliza mitihani, marufuku kuja mjini kutembea. Nendeni shamba mkalime, mkivuna, muuze mpate hela ya kulipia A-level na vyuo mtakavyochaguliwa.

Hakikisheni mnashinda mtihani, hata kwa bao la mkono.

Atakae chora zombie, kuandika rap, kukusanya booklet isiyojazwa, huyu ni jela moja kwa moja. Haiwezekani watu wazima tunaisoma namba kwa kuwa pesa yetu inakusomesha bure, halafu wewe ukalete mchezo.

Ni hayo tu. Haya, mkavune mlichokipanda.
 
Rekebisha heading ilete maana uliyokusudia
 
stress=panic=fail
don't get stressed
all the best on yout exams brothers and sisters
 
Ila serikali ijitahidi kuzuia uvujaji maana saa hizi mitihani ni kama open test kabisa hata maana inapoteza.
 
Back
Top Bottom