Kichofanyika Shinyanga ni Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar, au ni ziara ya kawaida ya Raisi?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Nilimsikia Mheshimiwa Raisi akidai kuwa Serikali imeanza kusheherekea/kuadhimisha sikukuu zake kwa staili ya mtawanyiko. Kwamba hata birthday inawezekana kusheherekewa sehemu mbalimbali.

Kwa maana hiyo hata kilichokuwa kinafanyika pale Shinyanga ni maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar!

. Niamejiuliza tu hivi kweli kilichokua kinafanyika jana pale shinyanga ni maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar au ziara ya Raisi kutoa shukrani kwa kuchaguliwa?

. Hivi Wana-Shinyanga jana walijua wamekuja kuadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar, au walikuja kumuona na kumsikiliza Mheshimiwa Raisi?

. Hivi kuna Kiongozi yoyote wa serikali na viongozi wa dini toka bara aliyezungumza lolote kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ukiacha Wale Wazanzibar wawili waliochomekea suala la Mapinduzi, tena kwa shida shida?

Mmmh!
 
Nikasikia asubuhi Star TV mtangazaji anasema rais ameazimisha mapinduzi kwa namna ya kipeeke.nijasiemea huyu mse.ngr anaweza kutupa hata neno moja tu alilozungumza rais kuhusu mapinduzi?
 
Ni kama ile ya kagera, ilikuwa ni kutoa pole ama ni ziara ya kukagua maendeleo mkoa wa kagera?
 
Ilikuwa ziara ya chama cha mapinduzi siyo mapinduzi yale. Mda wote anaongelea ndege kama vile wale wakulima wa shinyanga hawajawahi kuona ndege.
Jamaa kununua ndege kwake imekuwa bonge la story. Haamini kama amenunua as if ni personal issue.
 
Back
Top Bottom