KICHERE :MENEJA WA TRA ATAKAYEFUNGA BIASHARA YA MLIPAKODI KUKIONA

KICHERE :MENEJA WA TRA ATAKAYEFUNGA BIASHARA YA MLIPAKODI KUKIONA

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Kamishna Mkuu wa Kodi Nchini, Charles Kichere amewaagiza Mameneja wake wa TRA Nchini kutofunga Biashara ya Mfanyabiashara kwa sababu ya kutolipa ama kulimbikiza kodi na kudai atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa hatua Kali juu yake.

Kichere amesema hayo katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo kimojawapo cha Television Nchini na kusema kuwa zipo njia mbadala za kukutana na Mfanyabiashara na kukubaliana naye jinsi ya kulipa kodi kuliko kumfungia Biashara yake.

"Mimi naumia sana kuona Biashara zikifungwa sababu ya kodi kwani unapomfungia Mfanyabiashara unakosa hata kile kidogo hivyo nimewaagiza mameneja wangu kutofunga Biashara Bali wafanye mazungumzi na wafanyabiashara jinsi ya kulipana"
 
matamko yanayotolewa kwa vyombo vya habari yanakuwa tofauti na utekelezaji kwenye field.
 
Huyu Kamishna hatoshi kabisa hiyo nafasi maana amekuwa mzembe sana kwenye swala zima la kodi
 
Back
Top Bottom