Kichaa Cha Mbwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kichaa Cha Mbwa

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 16, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280  Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoambuklizwa kutoka kwa wanyama hadi binadamu kupitia kwa mate. Njia iliyo ya kawaida zaidi ni wakati ambapo mtoto ameumwa na mbwa. Hata mnyama anayefugwa nyumbani anaweza kuumwa na panya ama mnyama mwingine aliye na ugonjwa huu. Na wakati ambapo anamuuma mtu, atamuambukiza.

  Mnyama aliye tayari na kichaa cha mbwa kila mara yeye huonekana mgonjwa. Watu wengi hupata ugonjwa huu wakijaribu kumuhudumia mnyama mgonjwa. Mnyama wa mwituni anaweza kutulia kiasi cha kuonekana kama amefugwa au aliyefugwa kuwa na machachari mabaya hadi akaonekana kama mnyama wa mwituni. Dalili inayojulikana bayana ni kutokwa na ute kinywani. Mnyama mgonjwa hutokwa na mate mengi yanayotiririka tu.

  Baada tu ya kuumwa na mnyama mtu huenda asionyeshe dalili zozote za kuwa na ugonjwa huu. Ugonjwa huu huchukua kati ya siku ishirini na sitini kuoenyesha dalili zake. Hata hivyo, kumetokea visa ambapo dalili zimeonekana baada ya miezi au hata miaka baada ya mtu kuumwa.

  Mgonjwa anaweza kudhani eti ana homa kwani dalili za kwanza ni kuona kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kuhisi uchovu mwingi, kukosa hamu ya chakula na homa. Mtu huweza kuhisi uchungu au kujikuna mahali alipoumwa hata kama hicho kidonda kikiwa kimepona. Wao huwa na wasiwasi na hushindwa kupata usingizi. Hizi dalili huenea haraka na kumfanya mtu kukasirika haraka mno. Mtu hushindwa kujizuia kutenda matendo kwa nguvu ya misuli yake hutingikatingika. Hii ni kwa sababu hii sumu ya kuambukiza imeingila ubongo na kumfanya mgonjwa kushindwa kujidhibiti mwili na hisia zake. Kwenye hatua hii wagonjwa huogopa maji kiasi kwamba hata wanaweza kuogopa kunywa maji ya kunywa wanapopewa. Ubaya ni kwamba mgonjwa akifikia hali hii, huwa ameingiliwa sana na ugonjwa huu na unaweza kusababishia madhara makuu.

  Ingawa ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni nadra sana kuwashika watu, unaweza kuwa vigumu kuutambua mara moja. Iwapo utaumwa na mbwa au mnyama yeyote, ni muhimu uende upate matibabu mara moja. Tena hakikisha kuwa huyo mnyama ameshikwa na kufungwa ili akaguliewe iwapo ana ugonjwa wa kichaa. Iwapo utatibiwa vyema na dawa ya Immune Globulin pamoja na chanjo zinginezo, kuna uwezekano kuwa huenda usishikwe na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
   
 2. Mwansile

  Mwansile Senior Member

  #2
  Jan 27, 2015
  Joined: Jan 20, 2013
  Messages: 113
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  pamoja
   
 3. everlenk

  everlenk JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2015
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 11,190
  Likes Received: 4,871
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. merengo90

  merengo90 JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2015
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 6,465
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Nimepata kitu hapa
   
Loading...