Kichaa Cha Mbwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoambuklizwa kutoka kwa wanyama hadi binadamu kupitia kwa mate. Njia iliyo ya kawaida zaidi ni wakati ambapo mtoto ameumwa na mbwa. Hata mnyama anayefugwa nyumbani anaweza kuumwa na panya ama mnyama mwingine aliye na ugonjwa huu. Na wakati ambapo anamuuma mtu, atamuambukiza.

Mnyama aliye tayari na kichaa cha mbwa kila mara yeye huonekana mgonjwa. Watu wengi hupata ugonjwa huu wakijaribu kumuhudumia mnyama mgonjwa. Mnyama wa mwituni anaweza kutulia kiasi cha kuonekana kama amefugwa au aliyefugwa kuwa na machachari mabaya hadi akaonekana kama mnyama wa mwituni. Dalili inayojulikana bayana ni kutokwa na ute kinywani. Mnyama mgonjwa hutokwa na mate mengi yanayotiririka tu.

Baada tu ya kuumwa na mnyama mtu huenda asionyeshe dalili zozote za kuwa na ugonjwa huu. Ugonjwa huu huchukua kati ya siku ishirini na sitini kuoenyesha dalili zake. Hata hivyo, kumetokea visa ambapo dalili zimeonekana baada ya miezi au hata miaka baada ya mtu kuumwa.

Mgonjwa anaweza kudhani eti ana homa kwani dalili za kwanza ni kuona kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kuhisi uchovu mwingi, kukosa hamu ya chakula na homa. Mtu huweza kuhisi uchungu au kujikuna mahali alipoumwa hata kama hicho kidonda kikiwa kimepona. Wao huwa na wasiwasi na hushindwa kupata usingizi. Hizi dalili huenea haraka na kumfanya mtu kukasirika haraka mno. Mtu hushindwa kujizuia kutenda matendo kwa nguvu ya misuli yake hutingikatingika. Hii ni kwa sababu hii sumu ya kuambukiza imeingila ubongo na kumfanya mgonjwa kushindwa kujidhibiti mwili na hisia zake. Kwenye hatua hii wagonjwa huogopa maji kiasi kwamba hata wanaweza kuogopa kunywa maji ya kunywa wanapopewa. Ubaya ni kwamba mgonjwa akifikia hali hii, huwa ameingiliwa sana na ugonjwa huu na unaweza kusababishia madhara makuu.

Ingawa ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni nadra sana kuwashika watu, unaweza kuwa vigumu kuutambua mara moja. Iwapo utaumwa na mbwa au mnyama yeyote, ni muhimu uende upate matibabu mara moja. Tena hakikisha kuwa huyo mnyama ameshikwa na kufungwa ili akaguliewe iwapo ana ugonjwa wa kichaa. Iwapo utatibiwa vyema na dawa ya Immune Globulin pamoja na chanjo zinginezo, kuna uwezekano kuwa huenda usishikwe na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom