Kibwana Dachi amchana LIVE Wasira



Wassira ana mambo ya kitoto na uelewa wake ni mdogo mno!!!
 
Leo kabanwa Wasira,kesho akibanwa Slaa mtamponda mwandishi.
 
Kwani TYSON aliwahi kua Mpinzani??.

Baada ya kukorofishana ndani ya CCM alitua NCCR-Mageuzi, lakini alipobanwa mbavu kila upande akaanza kufilisika kimwili, kiuchumi na kiakili akaamua kulijisalimisha tena CCM na akapata uwaziri. Ugumu wa maisha aliopitia Wasira na uliomsukuma kutoka NCCR Mageuzi na kurejea CCM kamwe hawezi kusahau ..mzee alichanganyikiwa ikafikia wakati akitembea na viatu havina soli..
 

Is it true?
 
Dogo inaonekana historia ya Wasira huijui. huyu bwana aliupata Ubunge tangu mwaka 1975 akitoka katika ualimu wa TAPA. Baada ya hapo aliwahi kutumikia wadhifa mbalimbali ukiwemo mkuu Wa mikoa ya Mara na Pwani. Kuna kipindi aliondoka kwenda kusoma nje. Tatizo la wassira lilianza wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Mara. Alizidiwa kabisa alipokuwa mkuu wa mkoa wa Mara baada ya wananchi kumkataa mbele ya Rais Nyerere . Mzee Nyerere alikuwa kwenye ziara mkoani Mara na alikuwa amefika mjini Musoma kuongea na wananchi. Aliposimama Wassira kuongea kabla ya Mzee Nyerere kuongea , wananchi woote walisimama na kuondoka kikaoni. Hapo ndo akaua soo kwa kwenda kusoma nje ya nchi. Vyama vingi vilipoanza alijiunga na CHADEMA NA KUWACHACHAFYA SANA CCM na aliweza kumshinda aliyekuwa Waziri mkuu na Makamu wa Kwanza wa RAIS Mzee Sinde Warioba. CCM ilikata rufaa na Mzee Wassira akashindwa. Tangu hapo CCM ilimfanya kitu mbaya sana Wasira kwa kuahakikisha wanamhujumu kila sehemu. Kuanzia biashara yake ya kununua na kukoboa pamba mpaka kuwashawishi wapangaji wa kizungu (watariano ) waliokuwa wamepanga kwenye nyumba yake pale Manyamanyama wahame. Hali yake kiuchumi ikawa mbaya sana . akaamua kuwapigia magoti CCM na kurudi kundini.
 
Kibwana Dachi much know!
Ana ushabiki fulani bila kujijua.
 
Huko kwingine kama ni kweli au si kweli sijui, ila kuhusu Wasira kujiunga Chadema sio kweli, Wasira alikuwa NCCR wakati huo NCCR kweli kweli na hajawahi kujiunga na Chadema.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…