Ndugu zangu nimeona nianze kwa kuweka mstari huu wa Biblia kwa kuwa Magufuli anamweshimu Mungu na kwa kinywa chake amekuwa akikiri kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mimi pia nimependa niendelee kuwa mpenzi wa Mungu kwa kumwambia Magufuli ukweli unaotoana na neno la Mungu.
Mara zote Magufuli amekuwa akitaka sana maombi ya Watanzani bila kujali itikadi na imani zao, huku akijua wazi ndio waliomuweka hapo alipo kwa ajili ya kuwatumikia. Kwa bahati mbaya au kukusudia Magufuli ameanza taratibu kujivika moyo wa kiburi kiasi cha kusahau kuwa aliwekwa na watanzania ili awatumikie wala hajajiweka wenyewe. Ndio maana nikaanza na neo hili la
Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko."
Mithali 16:18
Ni jambo la kusikitisha sana kuona mtu aliyechaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia akiongea lugha la kiburi kama zile alizoongea siku ya kuweka jiwe la msingi pale Ubungo.
Mimi sikushauriwa na mtu kuchukua fomu kugombea Urais kwa hiyo siwezi kushauri cha kufanya, kwahiyo mimi ndie ninayejua nimuweke wapi mtu yeyote siwezi kupangiwa na yeyote. Hii ni lugha ya mtu mwenye kiburi ambaye amefika kiwango cha mfalme Nebukadneza wa Babylon aliyesema kuwa mimi ndie mfalme na mji huu niliujenga mimi, lakini Mungu alimpeleka porini akawa kama mnyama hadi pale aliponyenyekea tena baada ya miaka saba.
Lugha aliongea Magufuli ni ya kiburi maana kuna watu ambao wanalipwa kodi ya wananchi kwa ajili ya kumshauri, pia kuna viongozi wa kiroho wachungaji na mashehe ambao wanamshauri, wapo Marais wastaafu ambao pia wanatakiwa wamshauri, kwa maneno yake hayo amedhihirisha hawezi kukubali ushauri wa makundi yote haya kwa kuwa yeye ni zaidi ya raia wote wa Tanzania na ana akili kuliko watu wote. Hakika hiki ni kiburi ambacho Mungu hapendi kiongozi yeyote kuwa nacho.
Magufuli hahakisi tena moyo wa unyenyekevu aliowaonyesha watanzania wakati wa kampeni, amekuwa na lugha zenye viashirio vya kiburi kama hizi. Serikali ya Magufuli, Tanzania ya Magufuli, nataka niinyooshe nchi maana imevurugwa sana kila kitu kilikuwa hewa tu.
Jambo lingine la kushangaza amekuwa mtu ambaye hataki kuheshimu katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, mfano kuzuia mikutano ya kisiasa wakati katiba imeiruhusu ni kiburi kibaya sana kwenda kinyume na katiba.
Pia amekuwa mtu wa double standards kuna watu wamefukuzwa kazi ambao walibakiza mwaka mmoja kustaafu kwa kosa la kufoji vyeti, leo watu wanapiga kelele kwa kijana wake kukosa vyeti vya form four amesema achape kazi tu wala asiwasikilize. Juzijuzi Mwakyembe kafanya kosa la kuwataka watanzania wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa wasifunge ndoa kesho yake alikuja na tamko la kufuta kauli hiyo, ila la Makonda kuvamia ofisi za clouds na askari wenye bunduki ameona ni umbea wa mitandaoni.
Amekuwa mtu wa kutumia kauli kali za kutaka vyombo vya dola kutumia nguvu kwa raia, kiasi cha kutamani yeye angekuwa IGP
Magufuli jitafakari bado rehema za Mungu zipo ila kama hutaki Mungu hadhihakiwi.