Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Wilaya ya Kibondo mkoani kigoma imewanusuru zaidi ya watoto mia moja wenye ulemavu wa aina mbalimbali ambao walifichwa na kutelekezwa na wazazi kutokana na ulemavu wao na kusabaisha kukosa elimu pamoja na mahitaji mengine ya msingi.
Afisa elimu msingi wilayani humo joseph tirutangwa amemweleza mkuu wa mkoa wa kigoma brigedia jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliyetembelea shule maalum ya Nengo inayotoa elimu jumuishi pamoja na kukagua miradi kadhaa ya maendeleo, kuwa pamoja na shule hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali wamefanikiwa kuwachukua watoto hao ikiwa ni pamoja na wenye ulemavu wa ngozi,viungo na mtindio na kuanza kuwapa elimu huku uhamasishaji ukifanywa katika jamii ili wazazi wasiendelee kuwaficha majumbani watoto wenye ulemavu.