tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mgombea urais kupitia Chama cha MAKINI, Ndg. Coaster Kibonde, amesema endapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi hatopunguza matumizi ya Serikali wala mishahara na posho za watumishi wa umma. Alisema hatua hiyo inalenga kuongeza morali kazini na kuzuia tamaa ya rushwa ambayo mara nyingi huzaliwa kutokana na malipo duni. Kibonde alibainisha kuwa uwajibikaji bora na nidhamu katika matumizi ya fedha za umma ndizo zitakazosaidia kuleta ufanisi serikalini badala ya kupunguza haki za msingi za watumishi.
Akizungumza Septemba 2, 2025 katika mahojiano na Stanslaus Lambati kupitia Bongo FM, Kibonde pia aliomba Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) kutowanyang’anya magari waliyokabidhiwa kwa ajili ya kampeni. Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitawasaidia si tu katika kampeni, bali pia katika shughuli nyingine za kisiasa na kijamii zinazohusu chama chao.
Soma pia: Haya magari waliyopewa Wagombea Urais pamoja na madereva yanakuja na mafuta yake? Au hela ya mafuta inatoka kwenye fundraising?