Mbase1970
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 6,053
- 4,595
raia wema gani wanarushia polisi risasi mkuu?Wana uhakika? Isije ikiwa ni raia wema. Vinginevyo Good work
raia wema gani wanarushia polisi risasi mkuu?Wana uhakika? Isije ikiwa ni raia wema. Vinginevyo Good work
Polisi wametengeneza sinema feki pasipo kujua kuwa watanzania wa sasa wapo makini wanajua kila maigizoPolisi ni madaktari??Walijuaje wamekufa wakiwa njiani kuwapeleka hospitali??Inawezekanaje watu 4 wajeruhiwe halafu wote wafe wakiwa njiani kupelekwa hospitali?Kuna jambo hapa haliko sawa!
Waseme tu wamekutana na watu usiku wakawatandika risasi,basi!Hizo habari nyingine za kuungaunga zinaacha maswali mengiTatizo ni kuwa raia hawana imani tena na jeshi lao...
Njia panda ya Himo au Tinde Mkuu?Afadhali sasa waanze kufanya kazi sio kila siku wao wauwawe
Besides hawajaacha hata mmoja wa kuwasaidia upelelezi?
Ila hapo kwenye kudhani mmeniacha njia panda
Wana uhakika? Isije ikiwa ni raia wema. Vinginevyo Good work
Sasa kwanini warushiane risasi?Kwan polisi hawana smg? wametoa ofisin wakawaonesha kwamba wamekamata.. Tanua uwezo wa kufikiri nje ya box ndugu
Safi sana na ninakuelewa.Inafahamika vema kabisa kwamba maeneo mengi tu polisi wamekua wakipambana na halifu mbalimbali.
Kwa mfano kariakoo polisi walipambana Na majambazi yakiiba Kwa kutumia siraha, mbeya polisi waliwafukuzia majambazi walioiba pesa benki nk
Sasa inawezekana mkoa wa pwani kuna makundi hayo pia. Kutokana na mauaji yanayoendele Kwa Sasa ni dhahiri sasa kuna kundi jipya la uharifu linalowaua viongozi wa mitaa,vijiji,kata Na polisi.
Ndio maana taarifa inasema WANAOSADIKIWA, maana haijajulikana Kama ni majambazi wa kawaida tuliowazoea kila siku ama ndio wale wa mauaji ya kibiti.
Kabisa Mkuu, halafu tujiulize,Polisi ni madaktari??Walijuaje wamekufa wakiwa njiani kuwapeleka hospitali??Inawezekanaje watu 4 wajeruhiwe halafu wote wafe wakiwa njiani kupelekwa hospitali?Kuna jambo hapa haliko sawa!
Ukianza kuwarushia risasi polisi wewe utakua ni mtu wa amani kweli na hali kama ya kibiti. Hata kama tunawachukia mapolisi lakini tujaribu pia kuwa wakweli.Wanaodhaniwa? Kulikuwa na sababu gani iliyowafanya waonekane ni wauaji hadi na wao kuuawa?
Hili swala la polisi kujifanya wao ndio Judge, Jury and Executioner sidhani kama italeta amani.
Correction.
Ndio maana tunasema mnaanzisha sredi humu muwe na habari kamili. Sasa mtu mwanzon alileta akisema wanadhaniwa. Muda huu naona sredi iko tofauti na mwanzoni.
Usipost sredi kama bado huna uhakika.
Ngoja tusubiri kama watajibu mapigo.. counter attack iwe 1-1... maana dude limeamshwa hiloJeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
"Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji" Alisema Sabas.
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
Chanzo: ITV
iweje polisi wasijeruhiwe? hapo hakukuwa na mapambano bali waliwakamata wakawapeleka porini na kuwaua kisha wakazuga kuwa yalikuwa mapambano ya Nusu saa tu tena gizani? Wametengeneza sinema pasipo kutafakari kuwa watanzania wameamka uwezo kutambua mbinu zao,Sasa mkuu unadhani watu kama hao wanakubali kukamatwa wakiwa hai? Na umesikia jamaa walianza kurusha risasi. Hata S.W.A.T na FBI huwa wanawauwa watuhumiwa hasa kama ni cop killers.
MTU mchawi utamjua tu!Aiseee kumbe hawana evidence kamili bdo wanahisi tu,,,,
Aseeee ngoja wao zamu yao leo sasa
Yes sina tatizo na suala la uhalifu. Ninachosema ni kuwa Polisi kutumia maneno 'inasadikiwa' ni kutoa picha wasio na uhakika nayo kama ulivyosema (Hawana uhakika).Wamesema inasadikika au kudhaniwa kwa sab hawana uhakika kwa sab hawezi kusema wamefariki lkn cha msingi ni wahalifu.
Hahaha mkuu Tunduma mojaNjia panda ya Himo au Tinde Mkuu?
Kumbuka kuwa hairuhusiwi kwa RAIA kutembea usiku kwa maeneo hayo. Hawa walikuwa wanatembea usiku tena kama kikundi halafu wakiwa na silaha! Bado mnawatetea!Kama habari hii ni kweli lipo tatizo
Kudhania tu hakumfanyi mtu kuwa na hatia na adhabu!
Ni tatizo LA lugha tu, lakini mazingira ya kuwa na SMG usiku ni ushahidi tosha kuwa ni wahalifu!Wanaodhaniwa kuwa ni mauaji,hili picha bado asee