Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga, amesema watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria Kijiji cha Jaribu.
Lyanga amesema watuhumiwa hao walikuwa wakitoka Mkuranga kuelekea Kibiti kwa kutumia pikipiki wameficha fuvu hilo kwenye begi.
Amesema baada ya kufika katika kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki walisimamishwa na polisi waliokuwa doria eneo hilo na baada ya kuwakagua ndipo walipokuta fuvu hilo ndani ya begi.
Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali lilipotoka fuvu hilo.
Chanzo: Mwananchi