Kibamia au dushelelee, Ukweli ni upi?

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,534
4,185
++
Kumekuwepo na mjadala kuhusu ukubwa wa viungo vya unaofaa wakati wa mapenzi ili kumridhisha mwanamke.Wanaume wenye maumbile madogo (Kibamia kama inavyoanza kuzoeleka MMU) na wale wenye maumbile makubwa (Dushelelee kama tafsida ya MMU inavyoelezwa) wapo katika mitazamo hasi na chanya.
++
WANAWAKE WANASEMAJE
Wanawake wengi japo si wote,wanaamini kuwa maumbile makubwa ndio kila kitu katika mapenzi.Tena hata wanapokutana wao kwa wao hupeana habari juu ya uzuri wa maumbile makubwa.Na wale ambao wana wapenzi wao ama husaliti mahusiano yao kutafuta maumbile makubwa au hutumia dawa za kukausha maumbile ya kike ili wakati wa tendo la ndoa viweze kuwabana vema.
++
WANAUME WANASEMAJE
Wengi wao hawana jibu la moja kwa moja kuhusu maumbile yao.Lakini wapo wachache ambao hawalali,wanaendelea kutumia mizizi au dawa zinazotangazwa kuhusu kuongeza ukubwa wa maumbile ili wasi-aibike mbele ya wenzi wao.Na kuna wengine wameenda mbali kiasi cha kutumia pilipili !!
++
UKUBWA WA TATIZO
Tatizo ni kubwa na linaendelea kukua.Tena linachangiwa na wale wenye ujuzi wa kuongea na kutia chumvi mambo na wale ambao wana uzoefu mkubwa wa mapenzi toka mwenzi mmoja hadi mwingine.
++
UKWELI NI UPI?
Mtafiti wa mambo ya mahusiano na mapenzi Dkt Ed Wheat,anasema hilo husababishwa na watu kutojua na hofu isiyokuwa ya msingi hali inayopolekea kushindwa vibaya sana kimapenzi kuliko ukubwa wa viungo vyao.
Nae
Tim Lahaye ktk utafiti wake anasema kuwa
"..Ni kitu cha kushangaza sana kiasili lakini ni kweli kuwa,Kila Uume uliojaa damu unalingana na mwingine yaani urefu wa nchi sita hadi nane hata kama mtu mwenyewe ni mkubwa kiasi gani.."
Dkt David Reuben anasema kuwa "..Uume uliolegea unaweza kuwa na kipimo tofauti,kati ya nchi mbili hadi nne kwa urefu,utafiti bado unaendelea juu ya ni kwa nini zingine zinapungua sana kuliko zingine..."
Tim Lahaye yeye anawatoa wasi wenye maumbile madogo anaposema
"...Hata hivyo mwanaume anahitaji chombo cha uzazi chenye nchi mbili au tatu tu ili kuweza kufanya mapenzi vizuri sana,kwa sababu sehemu ya pekee ambayo imo ndani ya uke wa mwanamke,iliyo na uwezo wa kusisimuliwa kutokana na kuguswa au kusuguliwa ni ile inayotokea kwenye zile nyama za nje na kuingia ndani kiasi cha inchi mbili hadi tatu..."
++
FUTA MTAZAMO POTOFU
Hivyo basi wanawake waachane na imani kuwa maumbile madogo ya wanaume hayatawaridhisha na kama watabaki na mtazamo huo hawataridhika kweli maana "..kuridhika kwa mwanamke huanzia moyoni hadi akilini na kuenea mwili mzima.." anasema Dkt Naomi Gregoire mtaalam wa ushauri wa wanawake
Wanaume pia wajue kuwa hata mwanaume awe mfupi au mrefu kiasi gani,mnene au mwembamba,wa kijani au mweusi uume wake akiutunza vema akala vyakula vya asili basi imani kuwa hatamtosheleza mwenzi wake haina maana.Aache papara,amuingie vema mwenzi wake,acheze vema na umbile lake atashangaa mwenzi wake atataka kujiua akitangaza kumuacha
++
 
Watatobolewa kizazi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Yangu sijui ndo kibamia au dushelele, mie sielewi, saizi ya kati inaitwaje?
 
Back
Top Bottom