Kibaka apata Kipigo cha nguvu

Kibaka apata Kipigo cha nguvu

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,113
Reaction score
34,953

<center style="margin: 0px; padding: 0px; border: 0px none; outline: 0px none; vertical-align: baseline; background-color: transparent; text-align: left;"></center>

Bwana harusi mtarajiwa kumbe kibaka
*apata mkong'oto wa nguvu..soma kisa na mkasa kamili ndani....




Bwana harusi mtarajiwa kumbe kibaka
*apata mkong'oto wa nguvu

Na Issa Mnally
Kijana mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Shauri au Ustadh, ambaye ilielezwa kuwa hivi karibuni alipeleka barua ya posa maeneo ya Buguruni, alinusurika kuuwawa baada ya kumkwapua mtu simu maeneo ya Kariakoo, katika mitaa ya Aggrey na Max Mbwana na kisha kupewa kipigo cha 'mbwa mwizi'.

Wakati akipata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa raia wenye hasira, kijana mmoja alisikika akisema kuwa mwizi huyo anamfaham baada ya kuleta barua ya posa mitaa ya kwao Buguruni.

"Huyu jamaa namyaka kwa sana, hivi karibuni alileta barua ya posa pale kwa jirani yangu Buguruni, anatarajia kumuoa dada mmoja aitwaye Zainabu Abulrahman, loo..! kumbe ni kibaka?" alisikika kijana huyo akishangaa.

Baada ya kumsikia kijana huyo, mwandishi wetu alimvutia pembeni kijana huyo na kumuomba amuelezee vizuri ishu kamili, ambapo alimpa mkanda mzima na kasha kumuelekeza aliko mchumba wake.

Mwandishi alipofika nyumbani kwa mchumba wa jamaa, alishangazwa sana na habari kuwa mchumba wake ni kibaka na amepigwa vibaya na sasa anauguzia majeraha.

Dada huyo alikiri kutolewa barua ya uchumba na kibaka huyo lakini akasema kwamba hafahamu kuwa mchumba wake ni kibaka, yeye aliambiwa kuwa anafanya biashara ya samaki kariakoo sokoni.

"Hapana, Shauritanga siyo kibaka, kwani mimi alinieleza kuwa yeye ni mfanya biashara Sokoni Kariakoo, unaponiambia kuwa ni mwizi, nashangaa na ni habari mbaya sana kwangu" alisema dada huyo kwa huzuni kubwa huku akionyesha kukata tamaa.

Hata hivyo dada huyo hakutaka kuliongelea swala hilo kwa undani, kwani alitokomea ndani huku akiangua kilio kitu ambacho kilisababisha mwandishi wetu ashindwe kuteta naye kwa sana.

Kiapaka huyo, ambaye ilikuja kuelezwa baadae kuwa ni mzoefu wa kukwapua na kupewa kipigo mitaa hiyo, alikuwa akipigwa kwa kubadilishana ka mpira wa kona, lakini kutokana na roho ya paka aliyokuwa nayo, alisalimika japo aliondoka huku mwili ukiwa chap chapa kwa damu&#8230;!!!
 

Attachments

  • Kibaka1.jpg
    Kibaka1.jpg
    31.3 KB · Views: 204
  • Kibaka2.jpg
    Kibaka2.jpg
    28.6 KB · Views: 216
  • kibaka3.jpg
    kibaka3.jpg
    26.9 KB · Views: 203
  • kibaka4.jpg
    kibaka4.jpg
    22.4 KB · Views: 141
Hawa jamaa pindi wanapopewa vichapo huwa wanajifanya wanahitaji sana huruma...lakini ukimwachia tu siku ya pili anarudi kule kule.
 
40 ikifika haina kificho
Pia tujifunze kutochukua sheria mkononi
Linaweza kutoka kwa mwizi likaja kwa muibiwa
​
 
MziziMkavu,

Huu mtindo wa kuchangiana kwenye harusi kila mmoja ana njia zake. Jamaa anachangisha kwa nguvu. Hii ni hatari kwa dada zetu kwa kutofanya utafiti mnapoambiwa sehemu za kazi.
 
Hawa jamaa hiyo ndo dawa yao...wenyewe huwa wanangoja uende kazini ukataabike then wao wana subiri matunda tu! Hadi leo kaka zao wana TV yangu kubwa na laptop yangu, nilienda kazini, wenyewe wakaona huo ndo muda wa kuvunja geti na kuchukua chochote watakachokipenda....

Ningekuwa eneo la tukio, sio siri, ningeondoka na meno yangu mawili ya mbele....shuwaini....
 
Duh jamaa nadhani alikuwa anazichanga za mahali, labda baba mkwe kapanga mahali kubwa!!!!
 
Back
Top Bottom