Kibadeni, Mziray kuchukua Mikoba ya Mbulgaria??

Kipanga

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
676
34
Kuna habari zisizothibitishwa kuwa timu ya Simba wanafikiria kutumia kocha mzalendo kati Abdallah "King" Kibadeni au Syllersaid Mziray " Super Coach". Hali hiyo inafatia matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Simba imekuwa na matokeo yasiyoridhisha hali iliyopelekea timu hiyo mpaka sasa kuwa na ponti 13 ikishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya vodacom inayoendelea. Siku ya jumapili Simba ilitandikwa magoli 4-1 na Toto Africa ya Mwanza kitu kilichopelekea mtafuruku kutoka kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo wakitaka viongozi walioko Madarakani kujiuzuru. Simba inafundishwa na kocha kutoka Bulgaria Krasim Bezinsk....

Nakumbuka kibadeni alishawahi kufanyiwa fujo nyumbani kwake ilala na mashabiki wa Simba wakati fulani baada ya kuchapwa na Yanga...Tusubiri tuone!!
 
Back
Top Bottom