Kiatu cha mtoto kuning'inizwa kwenye gari

Sultan Kipingo

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
238
178
Wakuu habari,

Siku hizi si ajabu kupanda daladala au hata magari mengine ya biashara na kukuta kiatu kimoja cha mtoto kikining'inia aidha ndani au nje ya gari husika.

Naomba mnisaidie wenye ufahamu juu ya hilo, hivi kwanini huwa vinawekwa? Vina umuhimu gani kwenye gari?


1451294654368.jpg
 
Kwa jibu sahihi ungewauliza wahusika wa hiyo gari uloliona na kiatu,nijuavyo mimi mtoto wa abiria kimemvuka wanakiweka kwa kuning'iniza ili kama itatokea mwenye mtoto apande tena hilo gari basi akione kwa urahisi.
Wakuu habari,
Siku hizi si ajabu kupanda daladala au hata magari mengine ya biashara na kukuta kiatu kimoja cha mtoto kikining'inia aidha ndani au nje ya gari husika. Naomba mnisaidie wenye ufahamu juu ya hilo, hivi kwanini huwa vinaekwa? Vina umuhimu gani kwenye gari?
 
Mara nyingi watoto uvipoteza ndani gari bila wazazi kugundua,ufungwa pale ili muhusika akione kiurahisi
 
Watoto wlio wengi hupoteza viatu kwa hiyo watu huvitundika vile ili mwenye nacho akione kiurahisi hakuna maana nyingine ila wale wa kwenye nyaya za umeme huonyesha kuwa kuna pusha maeneo haya ni ni mbinu ya kizamani sana.
 
viatu huwavuka watoto bila wazazi wao kujua pale wanaposhuka kwenye gari so konda anapokiona anakitundika ili mzazi akione
 
Wakuu habari,

Siku hizi si ajabu kupanda daladala au hata magari mengine ya biashara na kukuta kiatu kimoja cha mtoto kikining'inia aidha ndani au nje ya gari husika.

Naomba mnisaidie wenye ufahamu juu ya hilo, hivi kwanini huwa vinawekwa? Vina umuhimu gani kwenye gari?


View attachment 313432
Utakuta wamehifadhi kitu ndumba na ngae,kwa ajiri ya imani kuwa wanajikunga na nguvu mmbadala,au kwa ajilri ya ybiashara.kwa sababbu kuna imani barabarani kuna mauzauza.Ukitaka uchokozi kiguse uone.
 
Viatu hivi hutavikuta kwenye daladala au juu ya nyaya za simu/umeme tu. Zipo hadi kwenye magari binafsi, hasa malori ya mizigo kama vile scania na fuso. sasa hapa jiulize kwenya haya malori ya mizigo kuna mtato alipanda akasahau kiatu? si sahihi. Hii ni imani fulani
 
Back
Top Bottom