Hahaha,Dunia ya sasa tunapaswa pia kujifunza tamaduni za watu wengine
Niliwahi kuona Colin Powell akifurahia kuoneshwa mbwa aliepewa jina lake
Sasa sisi waswahili mtu akikwambia nimempa mbwa wangu jina lako utaona nimekuheshimu au nimekudharau?
kwa waswahili mbwa ni kiumbe cha hadhi ya chini sana , ila hao wanamuona kama rafikiHahaha,
Bill Clinton alimpa mbwa wake jina la "Buddy", jina hilo lilikuwa la mjomba wake aliyempenda ambaye alikuwa amefariki muda si mrefu wakati huo.
Unaweza ku imagine mswahili umpe mbwa wako jina la mjomba wako aliyefariki muda si mrefu uliopita?
Mkuu hakuna kitu adhimu kama utamaduni na ustaarabu wa jamii. Kila jamii ina tunu zake ambazo ukizigusa unakosana nao, sisi tumekuwa tofauti kidogo ila wenzetu wako nazo hizo tamaduni zao. Usiwalaumu waarabu kwa kuwa sisi tamaduni zetu tunaziasi sana, Messi ana menejimenti na washauri anaowalipa ambao lilikuwa jukumu lao kutazama tukio hilo.Waliokasirika ndio wamechemka.
Messi ni football star. Kiatu ni football gear. Kutoa gear yake ni ishara ya heshima.
Utamaduni wa kuangaliwa hapo ni wa soka.
Dunia ya sasa tunapaswa pia kujifunza tamaduni za watu wengine
Niliwahi kuona Colin Powell akifurahia kuoneshwa mbwa aliepewa jina lake
Sasa sisi waswahili mtu akikwambia nimempa mbwa wangu jina lako utaona nimekuheshimu au nimekudharau?
Mkuu hakuna kitu adhimu kama utamaduni na ustaarabu wa jamii. Kila jamii ina tunu zake ambazo ukizigusa unakosana nao, sisi tumekuwa tofauti kidogo ila wenzetu wako nazo hizo tamaduni zao. Usiwalaumu waarabu kwa kuwa sisi tamaduni zetu tunaziasi sana, Messi ana menejimenti na washauri anaowalipa ambao lilikuwa jukumu lao kutazama tukio hilo.
Hao wataalamu walitakiwa wamwambie Messi hiki hakifai kwa hawa watu, atafute njia zingine manake anazo sports gear nyingi sana. Kma unakumbuka suala la Mascerano alivyokumbwa na suala la kodi, yeye alisema kuna watu amewaajiri na lilikuwa jukumu lao kulipa kodi na yeye binafsi hahusi na adhabu itakayotolewa.
mimi sitamlaumu Messi, kwa kuwa alikua na lengo zuri tu,watu wengine vichwani kumejaa kamasi tupu,unalazimishaje misri apende tamaduni za messi?huyo messi akifanyiwa vitendo ambavyo si utamaduni wake atachekacheka?wabongo sijui tuna nini sisi,au chuki tu kwa wamisri?
Samahani mkuu, katika nchi za kwanza duniani kuuonja ustaarabu ni Misri. Hawa watu wana ustaraabu mkongwe sana na wanauheshimu sana, unaweza kuona ni waarabu waliopo Afrika lakini kwenye duru za kiarabu Misri ni moja kati ya nchi zenye heshma kubwa sana.mimi sitamlaumu Messi, kwa kuwa alikua na lengo zuri tu,
halafu pia mbona wachezaji wa Raja Casablanca ya Morocco (ambao ni waarabu) walishang'ang'ania viatu vya ronaldinho ili wakaviweke kama ufahari? kwa hiyo tamaduni za hawa watu hazipo clear
Ronaldinho booted out of the Club World Cup by Raja Casablanca players
sasa kama waarabu wanaona kiatu cha mtu ni kama tusi kwao kwa nini waling'ang'ania hicho kiatu cha dinho? au hawa walivunja tamaduni?Samahani mkuu, katika nchi za kwanza duniani kuuonja ustaarabu ni Misri. Hawa watu wana ustaraabu mkongwe sana na wanauheshimu sana, unaweza kuona ni waarabu waliopo Afrika lakini kwenye duru za kiarabu Misri ni moja kati ya nchi zenye heshma kubwa sana.
Kama utakumbuka mwanzoni ilikuwa ni adimu sana kuona mchezaji wa Misri akicheza ligi nje ya Misri. Yote ile ilikuwa ni kuonyesha wenyewe ni bora sana. Sasa kwa hili la Messi linafungua hisia zingine kwa Waarabu wa Misri, wanaona Messi hajawatendea haki, kwa kuwa kama ni sportsgear mbona zipo nyingi ukiachilia mbali kiatu! Pole sana mkuu.
Mie nazungumzia waarabu wa Misri weye unawasema waarabu wa Morocco, sasa tutaelewana? Nimeshakueleza hapo juu jinsi waarabu wa Misri walivyo tofauti na Bedouins!sasa kama waarabu wanaona kiatu cha mtu ni kama tusi kwao kwa nini waling'ang'ania hicho kiatu cha dinho? au hawa walivunja tamaduni?
Mzee kajaribu uone!kwa hiyo waarabu wanao mind ishu ya viatu ni wa misri tu?