Habari ndugu zangu, toka mwaka Jana nimekuwa nakabiliwa na tatizo la oxygen kuwa chini (circulating) kila nikienda hospitali nikipimwa iko 82 mpk naogopa Yani,nilikua naishi mkoa wa joto mwaka Jana nikahamia mkoa wenye baridi sn na baridi inanishindwa hivyo nimekua nikiumwa nimonia Mara kwa Mara.
Sasa hili la oxygen linaniumiza sn kichwa kila nikipwa ikiwa ndogo nawekwa kwenye mashine ya oxygen ikikaa sawa wananiruhusu. Naombeni kujua kwanini napitia hii Hali na nifanyaje ili iache
Pole kwa kuumwa.
Ni ngumu kulifafanua vyema tatizo lako, ingawa ni vyema kutanabaisha hizi zinazoitwa nimonia za mara kwa mara.
A: Hii, inaweza kuwa ni magonjwa yanayoingilia uwezo wa kutanuka na kusinyaa kwa viriba vya hewa(constrictive palmonary diseases) au kusababisha kunenepa kwa eneo linalohusisha mchakato wa kuhamisha damu kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye damu(basement membrane hypertrophy).
B: Hii inaweza kuhusisha pia tatizo la mishipa ya damu/mfumo toka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu pamoja na moyo wenyewe.
Lakini, pia kuna haja ya kujua kama:
1: Kuna watu kwenye familia wana tatizo la allergy yoyote au ugonjwa wa kifua wa mara kwa mara.
2: Kazi ulizowahi kufanya tangu mdogo mpaka leo.
3: Uzito wako/obesity hypoventilation syndrome
4: Umri.
NB: Kama unaweza kumpata daktari bingwa wa mapafu (palmonologist) ingekuwa ni vyema zaidi.
Pamoja na CT pendekezwa hapo juu, ni muhimu kufavya vipimo vya kuangalia uwezo wa kutanuka kwa mapafu na uwezo wa kutoa hewa nje. (Peak flow meter vs spirometry)
Ukimkosa Palmonologist, hata daktari bingwa wa magonjwa ya ndani/ physician pia anaweza kufanya vyema.