Kwanza katika blog ambazo nilikuwa naziamini kiasi kwamba siwezi pitisha siku bila kuipitia ni blog ya bwana michuzi, ila kwa sasa najionea kichefuchefu kabisa kuifungua kwani najua lazima takutana na habari na picha za watu wa ccm zaidi ya asilimia 80. Ule usemi wake wa sibagui sichagui atayenizika simjui ni danganya toto tupu, kwani ameshindwa kabisa kuficha hisia zake kuwa yeye ni kada wa kutumainiwa wa ccm.