KI Moon: Migiro ameomba kupumzika akajenge nchi yake!

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo, Asha Rose Migiro ameomba mwenyewe kustaafu.Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijiji New York, Marekani, Ki Moon alisema hata hivyo Dk Migiro ataendelea kuwapo kwenye ofisi za umoja huo, akiratibu shughuli mbalimbali hadi Juni mwaka huu.

Alisema mbali na Dk Migiro, mwingine aliyeomba kuacha kuutumikia umoja huo ni Vijar Nambiar ambaye ni Mkuu wa Ofisi yake.

“ Kama mlivyotangaziwa mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa kufanyika katika nafasi za watendaji waandamizi. Ningependa kuongezea na kuwajulisha kwamba, Naibu Katibu Mkuu, Dk Migiro na Vijar Nambiar wamewasilisha kwangu maombi yao ya kutaka kuachia nafasi zao ili kuniruhusu kuunda timu mpya ya maofisa waandamizi nitakaofanya nao kazi katika awamu ya pili ya uongozi wangu,” alisema Ki Moon.

“Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Naibu Katibu Mkuu, Dk Asha- Rozi Migiro, kwa uamuzi wake huo, na kwa kazi nzuri na ushirikiano mkubwa na usio na shaka wala doa alionipatia katika kipindi chote cha miaka mitano iliyopita akiwa msaidizi wangu wa karibu,” alisisitiza.

Alisema Dk Migiro alimpa ushirikiano mzuri mno na kumshauri kwa busara huku akijituma kwa uadilifu mkubwa katika kukabiliana na changamoto nyingi zinazoukabili Umoja wa Mataifa.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, aliyasema hayo baada ya kuainisha mpango kazi na vipaumbele vyake katika miaka mitano ya muhula wa mwisho ya uongozi wake Kwa mujibu wa Ki Moon watendaji wengine watakaondoka ni wa Idara za Utawala, Maendeleo, Huduma za Mikutano, Habari, Ofisi ya Upokonyaji wa silaha, na Mshauri wa Masuala ya Afrika.

Wengine ni wasimamizi wa Idara za Uchumi za Afrika na Ulaya, waratibu wa mifuko ya maendeleo na Idadi ya watu UNDP na UNFPA.

Mwananchi
 
Wakubwa nao wanalugha laini ya kuwasilisha maamuzi yao! Hii yote ni kuondoa kiwingu cha maswali juu ya maamuzi yaliyochukuliwa.
Hata hivyo tunakukaribisha nyumbani Mama Migiro, huku site wanasema unasubiriwa wewe ili Mkuu afanye mabadiliko ya baraza la mawaziri. Sijui umeshajua majukumu yako mapya!? Naona KI Moon anasema umeamua kuja kujenga nchi yako!
 
akajenge nchi yake??huyo Kin Moon hajui huyo Migiro alikuwa anaijenga kabla hajamchukua??kuna jipya atakuja nalo au ni yale yale???
 
Hivi huyu mama yuko kwenye mtandao upi? Je atahimili minyukano iliyopo sasa? Yeye aje tu ila aangalie asijeakapata stroke na mapresha kwa siasa zetu sikuhizi mpaka ukajutia uamuzi wa kondoka UN. Ningekuwa namfahamu ningemshauri tu ubakie huko huko maana huku anakuja kuzeeka kabla ya wakati na tutajua kashfa zake kibaaaaao kabla hata hajaanza mchakato!
 
Ni utaratibu wa kawaida pale UN muda wa katibu mkuu ukiisha wote mna resign mnaomsaidia ili ajenge timu mpya. Sema wabongo huwa hawajazoea haya mambo ndo maana wanamshupalia Migiro.
 
Ni utaratibu wa kawaida pale UN muda wa katibu mkuu ukiisha wote mna resign mnaomsaidia ili ajenge timu mpya. Sema wabongo huwa hawajazoea haya mambo ndo maana wanamshupalia Migiro.

Sio kweli, wakina Lord Malloch Brown walikaa sana wakati wa Kofi Annan. Ban Ki-Moon anampa anamtunzia hesham tu huyu mama. Migorpo kapiga sana mguu kwa matonya wenziwe (African Union) ili wamuunge mkono aendelee na nafasi yake. But Ban was having none of that!

Migiro alifanya makosa huko nyuma pale alipojisahau na kuanza ku-shuttle New York -Bongo. Kila kukicha huyu mama alikuwa bongo, mara anafungua warsha (tena warsha za kawaida kabisa) mara anaongea na wabunge, mara zanzibar. Ili mradi alijiaminisha kuwa yeye ni rais mtarajiwa. Lakini alivyoona mitandao inasambaratika akili zikamrudia - too late. Sasa arudi hapa apambane na vumbi na mgao wa umeme. Na urais hapati labda uwaziri.
 
Ni utaratibu wa kawaida pale UN muda wa katibu mkuu ukiisha wote mna resign mnaomsaidia ili ajenge timu mpya. Sema wabongo huwa hawajazoea haya mambo ndo maana wanamshupalia Migiro.

Acha uzushi. Kwamba muda wa Katibu Mkuu ukiisha wote mnaresign. Mbona yeye Ki-Moon hajaresign na anaendelea? Au ni Katibu Mkuu yupi unayemuongelea? Maza kapigwa chini politely.
 
mtandao wa mafisadi,ni mbadala wa Lowasa kama Nec ikionyesha shingo upande basi nguvu zote zitahamishiwa kwake ili awe Rais 2015,lakini ukweli ni kwamba evaluation aliyofanyiwa mwaka jana based on result ameonekana kuwa hajafanikisha kitu chochote kwenye UN,nakuombwa kujihudhuru badala ya kufukuzwa,matokeo ni kwamba she is to processal based and not result oriented wakati UN inataka result oriented persons.Mama karibu nyumbani.
 
Ni rahisi. Alex Fergusson alipomchoka berbatov akasema berbatov ameomba kuhama ili apate nafasi ya kucheza full time na ili ajenge kikosi kipya cha vijana. Kwa maana pana uwezo ukipiungua ni lazima uondoke
 
Wana bodi Migiro ali under perform! na kama aliomba ku resign ili akapumzike kama alivyosema moon hata akirudi nyumbani asijiingize kwenye siasa ili apate nafasi ya kupumzika. huyu mama aliboronga kishenzi kwenye hiyo taasisi kubwa ulimwenguni kipindi kile aliondoka hapa na majigambo na ile minywele yake ya Afro utafikiri ni Tigo thumuni
 
Pangolin unanchekesha xana,eti nywele za tiGO thumni!
Wana bodi Migiro ali under perform! na kama aliomba ku resign ili akapumzike kama alivyosema moon hata akirudi nyumbani asijiingize kwenye siasa ili apate nafasi ya kupumzika. huyu mama aliboronga kishenzi kwenye hiyo taasisi kubwa ulimwenguni kipindi kile aliondoka hapa na majigambo na ile minywele yake ya Afro utafikiri ni Tigo thumuni
 
Msitegee mengi kwani yako wapi ya Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka, naye si-alikuwa UN-HABITAT kaongeza nini? mbona hata jimboni mwake wanalia kilio cha MBWA kwa kumchagua na kupita Bila kupingwa, wakina mama wakichoka wanachoka vibaya, Angalia yule mama wa UKELEWE, tuje na Bi-Kiroboto hapo ndio utapata jibu kuwa hii kasi ya kizazi cha Dotcom hawakiwezi.
 
JK ni raisi weak sana! Yaani yeye hawezi kuendelea na mipango yake, ikiwapo re-shuffle mpaka asubiri walioko nje! Huyu mtu ni weak sijawahi ona...

Kwa hiyo running a country can wait....Only in TZ!!
 
Huyu Dr Migiro kasi ya kimataifa imemshinda hasa utendaji sasa ndiyo anataka eti arudi awe rais wetu 2015??????????Tumekwisha hata kama Tanzania 2015 for women lakini siyo huyu bora tumpe Liberata Mulamula
 
sio kweli, wakina lord malloch brown walikaa sana wakati wa kofi annan. Ban ki-moon anampa anamtunzia hesham tu huyu mama. Migorpo kapiga sana mguu kwa matonya wenziwe (african union) ili wamuunge mkono aendelee na nafasi yake. But ban was having none of that!

Migiro alifanya makosa huko nyuma pale alipojisahau na kuanza ku-shuttle new york -bongo. Kila kukicha huyu mama alikuwa bongo, mara anafungua warsha (tena warsha za kawaida kabisa) mara anaongea na wabunge, mara zanzibar. Ili mradi alijiaminisha kuwa yeye ni rais mtarajiwa. Lakini alivyoona mitandao inasambaratika akili zikamrudia - too late. Sasa arudi hapa apambane na vumbi na mgao wa umeme. Na urais hapati labda uwaziri.

kweli kabisa mkuu wewe si mdogo wake ban ki-moon na uko jikoni kabisa so unajua kila kitu
vipi kaka yako anaendeleaje na michakato?
 
Sio kweli, wakina Lord Malloch Brown walikaa sana wakati wa Kofi Annan. Ban Ki-Moon anampa anamtunzia hesham tu huyu mama. Migorpo kapiga sana mguu kwa matonya wenziwe (African Union) ili wamuunge mkono aendelee na nafasi yake. But Ban was having none of that!

Migiro alifanya makosa huko nyuma pale alipojisahau na kuanza ku-shuttle New York -Bongo. Kila kukicha huyu mama alikuwa bongo, mara anafungua warsha (tena warsha za kawaida kabisa) mara anaongea na wabunge, mara zanzibar. Ili mradi alijiaminisha kuwa yeye ni rais mtarajiwa. Lakini alivyoona mitandao inasambaratika akili zikamrudia - too late. Sasa arudi hapa apambane na vumbi na mgao wa umeme. Na urais hapati labda uwaziri.

FJM,

..Malloch alitumikia kwa miezi kama 8 hivi kabla ya kuachia ngazi akifuatana na Koffi Annan.

..mtangulizi wake aliserve kwa kipindi cha miaka 5 au 6.

..wenzetu hawana utaratibu wa kungangania sehemu moja kwa muda mrefu.

..hata Maraisi au in this case Katibu Mkuu UN ni lazima wabadilishe timu ya wasaidizi ikiwa wata-serve term zaidi ya moja. Hatua kama hizo humsaidia mhusika kuleta mawazo mapya ktk uongozi wake.

NB:

..UN Deputy Secretary General huwa wanapangiwa majukumu yao moja kwa moja na Secretary General mwenyewe.

..kwa msingi huo Dr.Migiro asingeweza kusafiri popote pale bila baraka za ofisi ya Ban Ki Moon.
 
Back
Top Bottom