Nsumba-ntale
Member
- May 24, 2026
- 15
- 80
Ukiangalia hali na mwenendo wa siasa za Tanzania, hususani inavyochukuliwa na wenzetu huko ughaibuni, ni wazi viashiria vya mageuzi ya kulazimishwa, vinamea
Wanao sababisha viashiria hivyo kumea ni Mange, Maria na wenzao wasio choka kushirikisha taarifa ima hasi ama chanya zihusuzo matukio yaendeleayo nchini Tanzania
Wengi kwa mfano, waliwabeza na hata kuwa tweza hao ndugu kwa walichokifanya na wanacho endelea kukifanya. Mda mrefu ndugu zetu hao wamekuwa wakihanikiza Nchi za Ulaya na mshirika wao Amerika, waishinikize Mamlaka ya Tanzania iwajibike kwa matendo yake wanayo-yaona ni kinyume cha haki za kibinadamu
Nionavyo, dhahili wapambanao wanaelekea kufaulu kwa wanacho kisimamia. Kwa Nchi za magharibi kuanza kuonyesha nia ya kuitungia sheria na vikwazo Nchi ya Tanzania, tayari kelele zao zimeshasikika na kufanyiwa kazi
Wahenga walinena, hata mbuyu ulianza kama mchicha, wasipuuzwe!