Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,454
- 32,980
KHITMA YA JUMA MWAPACHU
Ndugu na jamaa leo walikusanyika nyumbani kwa Juma Mwapachu kusoma khitma.
Mtume SAW kifo kinatosha kuwa mawaidha.
Kwangu binafsi kuwa kwenye nyumba ile kulirejesha kumbukumbu nyingi za furaha nikiwa na marehemu ukumbini kwake tukizungumza mengi.
Halikadhalika katika hadhira ile niliwaona watu wengi ambao kwa namna moja au nyingine walirejesha fikra zangu kwa marehemu.
Katika wengi tuliohudhuria khitma hii sisi wakati wa uhai wake Juma Mwapachu alikuwa kaka mkubwa kwetu kwa kila hali.
Juma Mwapachu alitutangulia sisi kwa kila kitu kuanzia kuingia Chuo Kikuu hadi katika ajira iwe serikalini, shirika la umma au binafsi.
Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa University of East Africa wakati sisi wengi wetu tuko sekondari.
Katika niliowaona pale khitmani waliosoma University of East Africa alikuwa Mohamed Ismail na Prof. Issa Shivji.
Waliobakia niliowafahamu walisoma Dar es Salaam University na hatukulikuta hata vumbi lake pale chuoni.
Juma Mwapachu kwa wengi wetu tuliokuwa pale kama nilivyosema alikuwa kaka.
Sasa nawaangalia wale wa rika la kaka Juma Mwapachu Yusuf Kalala, Mohamed Ismail, Prof. Issa Shivji wote wamejikusanya wamekaa pamoja.
Miaka imekwenda lakini wanapendeza.
Katika hawa kwangu mimi kila mtu ana historia ya yake ya kupendeza.
Issa Shivji alitikisa bongo za wasomi wengi wa wakati ule kwa kitabu chake, "Class Struggles in Tanzania."
Kwa nyakati zile kitabu hiki kilikuwa kitabu cha kutisha.
Kaka Yusuf Kalala mwanafunzi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School kipi asichokijua kuhusu Dar-es-Salaam?
Siku moja namwambia Bi Bahai keshafariki.
Akaniambia yu hai.
(Kulikuwa na Bahia wawili na wote maarufu - Bi. Bahia Lumelezi na Bi. Bahia mke wa Sheikh Mzee Ali Comorian. Mmoja katika hawa ndiye aliyekuwa kutangulia mbele ya haki).
Juma Mwapachu alipanda mabega ya Mohamed Ismail kukwea mlingoti uliokuwa unapeperusha Union Jack kuiteremsha chini katika maandamano dhidi ya Uingereza kutochukua hatua Ian Smith alivyotangaza uhuru wa Southern Rhodesia yaani "Uniletaral Declaration of Independence," maarufu UDI.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu walikuwa wameandamana kutoka Mlimani kuja Ubalozi wa Uingereza.
Wanafunzi walikuwa wamejaa ghadhabu.
Huu ulikuwa mwaka wa 1965.
Juma Mwapachu na Mohamed Ismail wote wanafunzi wa sheria walikuwa vijana wadogo.
Kisa hiki alinihadithia Mzee Ahmad Rashaad Ali aliyeshuhudia tukio hilo kwa macho akiwa na akiwajua hawa watoto kama alivyopenda kuwaita.
Mzee Rashaad akisema Juma Mwapachu alikuwa akiendeleza vile vita vya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu dhidi ya Waingereza wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Tulipokuwa tunachukua chakula akanijia mtu akaniuliza kwa nini nimekataa kuzungumza.
Nilikuwa nimesimama na Chief Edward "Ted" Makwaia wa Siha, Usukuma.
(Ted ndiye aliyenijulisha kwa Juma Mwapachu mwaka wa 1967).
Nilimjibu kuwa sikukataa ila nasaa walizotoa masheikh zetu zilitosha.
Lakini kama ingekuwa hadhira nyingine si khitma ningeeleza kisa hiki cha kutunguliwa bendera ya Mwingereza Juma Mwapachu kapanda mabega ya Mohamed Ismail kuuparamia mlingoti wa Union Jack.
Lakini kisa hiki ningekieleza kwa urefu kama alivyonihadithia Mzee Rashaad kuanzia jana yake Mzee Ahmed Rashaad akiwa Deputy Permanent Secretary Information alipokwenda nyumbani kwa Mwalimu Nyerere kutaka kauli yake kuhusu tatizo la Rhodesia ili Wizara ya Habari itoe "Press Release."
Rashaad alikumkuta Mwalimu nyumbani kwake anazungumza na Dossa Aziz na Lucy Lameck.
Kuna stori kubwa Nyerere alimhadithia Mzee Ahmed Rashaad Ali.
Kushoto: Wakili Mohamed Ismail, Shariff, Yusuf Kalala, Prof. Othman Chande na Ali Boxer