Khamis Mgeja: Samwel Sitta lazima afukuzwe CCM

Khamis Mgeja: Samwel Sitta lazima afukuzwe CCM

Amna msafi ndani ya ccm sita arudi ccj waliyoianzsha wakakimbia kivuli chao...jasri anayeogopa kivuli chake anazeeka vbaya
 
Amna msafi ndani ya ccm sita arudi ccj waliyoianzsha wakakimbia kivuli chao...jasri anayeogopa kivuli chake anazeeka vbaya ...SITA NAYE MCHAFU NA MWIZI ATUPE BREAKDOWN YA HIZO PESA TSH MILION 25 KWA MSHAHARA UPI WAKAT KNA MAGUFULI ALIODAI WAMEMPA MILION TANO WAMEMKANA MWIAZI MKUBWA HUYU
 
Hamis Mgeja yupo kundi gani linalotaka Urais 2015?. Upo kwa Membe, Migiro, Lowasa au upo kwa Steven Wasira?
kundi la lowassa,Naona kauli ya Mukama itatimia mgombea rais ccm atatoka nyanda za juu kusini mwanamke Anna Makinda
 
Huwezi kuwa funza ndani ya mzoga fisi akaula mzoga bila funza kuathirika.huyu sita ni sawa na funza.akitaka akafufue ccj.huyu mzee ni mmbeya na mfitini tena mnafiki.huwezi kupewa nchi kwa fitna kama za jk.mwl,mwinyi na mkapa hawakuwa hivyo ila imeanzia kwa baba riz.sasa tunasema hatudanganyiki....
 
Hamis Mgeja yupo kundi gani linalotaka Urais 2015?. Upo kwa Membe, Migiro, Lowasa au upo kwa Steven Wasira?
Huyu ana urafiki wa kuchanjia na Lowasa. Hapo alipo hafanyi kazi ya chama kwa kumshambulia Sitta, bali anafanya kazi ya Lowasa
 
"Kuna wakati tulikaa tukataka kumnyang'anya hata kadi"

Sasa huyo mzee Mgeja mbona anatoa siri za vikao nae? Duh wazee wa hicho chama!

Kwanza mbona asipeleke malalamiko ndani ya chama?Ukuwadi wa Mafisadi tu
 
Naona ni mbinu chafu hizo za magamba na makundi ya kuhujumiana si.Sita wala Mgeja wanapaswa kuogopwa kama ukoma. Iweje mgeja amuongelee mwanachama mwenzake wakati yeye si msemaji wa chama ni mwenyekiti tena wa Mkoa fulani. Ilitakia tusikie kauri kutoka kwa mtu maalumu anayekisemea chama ambaye ni katibu wa habari na uenezi

Mgeja ni kundi la E Lowasa ndiyo maana amerap sana. Makundi hayo yanachafuana.
 
Sasa hapa nashindwa kuelewa kati ya Mr.Rais na mgeja nani mkubwa kimaamuzi? Jk alisema wanaotaka nafasi ya urais 2015 waanze kupitapita lakini siyo kwa fujo alisema maneno haya dodoma alipokuwa anaongea na wabunge wa chama tawala,mgeja anasema itahatarisha chama ,mbona wanajichanganya?
Kweli CDM moto wenu unatisha.itafika mahali waheshimiwa wa magamba watashindwa kuziamini hata kauli zao wenyewe,maana hawana uhakika na matokeo ya kauli hizo.Na hii ni dalili ya kutojiamini ambayo inaashilia kupoteza uwezo wa kushika dola.
 
wote walewale! Mgeja anapinga rushwa anayoiongelea sitta hata rais ameziongelea hadharani. Hafai mngeja.
 
SIKU chache baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kutangaza timu inayoundwa na kundi lake kuwania urais 2015, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema chama hicho kinatakiwa kumchukulia hatua za kinidhamu kwa sababu anahatarisha uhai wa chama.

Alisema, kama chama kitamuacha aendelee kutoa kauli zinazohatarisha uhai wa chama, CCM itajiweka katika mazingira mabaya kisiasa pindi wapinzani watakapoanza kuchambua kauli hizo.

Kauli hiyo ya Mgeja, aliyoitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari, imekuja ikiwa ni siku chache tu tangu Sitta aitaje timu inayoundwa na kundi lake kuwania ukuu wa dola mwaka 2015.

Alisema wanaounda timu hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, ambaye hata hivyo amekana kuwamo kwenye timu hiyo.

Jana akimzungumzia Sitta, Mwenyekiti huyo wa CCM, Mgeja alimshushia tuhuma nyingi akimwita mkorofi, mlalamishi na kwamba anaonekana wazi kukihujumu chama.

Mgeja pamoja na mambo mengine, alimshutumu Sitta kuwa alianzisha CCJ akiwa ndani ya CCM, kisha akataka kuhamia Chadema akiwa ndani ya CCM na yote hayo chama kiliyajua na kumwacha.

Alisema Sitta yeye ni waziri, lakini kuna wakati alikaririwa akisema kwamba, Serikali iwaombe radhi wananchi kwa sababu ya mgawo wa umeme, baadaye akasema maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezekani na sasa amekaririwa hivi karibuni akisema Rais Kikwete alimhujumu kwenye uspika.

“Yaani anajiamini kiasi cha kuanza kumchokonoa hata Rais Kikwete, wakati akijua kwamba mambo anayoyafanya yanakwenda kinyume na mtazamo wa chama.

“Hivi huyu ni mtu gani asiyetosheka, kila wakati analalamika wakati yeye ni waziri na ana nafasi kubwa ya kupeleka malalamiko yake kwenye chama ili yakafanyiwe kazi.”

Alisema kama Sitta anaona yuko kwenye basi lenye abiria asioendana basi aondoke na kuhoji anafanya nini ndani ya CCM wakati anaonekana wazi kwamba haridhishwi na mwenendo wa chama na Serikali.

Mgeja pia alimtaka Sitta kwenda TAKUKURU kama anaona kuna rushwa ndani ya chama, au kama kuna wezi aende polisi na kama anaona kuna wahalifu, basi aende mahakamani.

“Lakini huyu mzee lazima chama kimchukulie hatua, huyu ni mzigo, kama hatadhibitiwa atakiharibu chama kwa sababu anaonekana ana ajenda ya siri,” alisema.

Mgeja aliitaka Kamati ya Maadili ya chama inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula, imjadili ili ijulikane ana ajenda gani.

Alisema kwa upande wake katika kikao cha NEC kijacho, atawasilisha hoja binafsi kutaka Sitta ajadiliwe.

“Yeye anajifanya ni msafi wakati mambo yake mengi tunayo, kwani hata alipopata uspika anaouota hadi sasa, alibebwa, tena kwa kampeni kali kweli kweli. Hivi, kwa nini asiwe kama mzee Msekwa (Pius Msekwa) ambaye baada ya kushindwa uspika alinyamaza kimya?” alifoka Mgeja.

Kwa mujibu wa Mgeja, kitendo kinachofanywa na Sitta ni cha hatari kwa uhai wa chama na kwamba kama isingekuwa huruma ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete, angeshafukuzwa uanachama wa CCM.

“Kuna wakati tulikaa tukataka kumnyang’anya kadi na aliokolewa na Mwenyekiti wetu, lakini pamoja na kusamehewa, bado hatulii, anaendeleza mambo yake ya ajabu ajabu,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Sitta ya wiki hii aliyoitoa akiwataja Magufuli, Membe na Dk. Mwakyembe kwamba ni wasafi, alisema ni ya kibaguzi, kwa kuwa waliotajwa ni Wakristo, wala hakuna Muislamu hata mmoja.

“Aliowataja wote hao akiwa kanisani ni wakristo, wala hakuna Muislamu, wote hao ni wanaume na hakuna mwanamke, pia hao wote ni kutoka Tanzania Bara na inavyoonekana Unguja na Pemba hakuna watu safi.

“Sasa mtu kama anadiriki kusema uongo, tena madhabahuni, ana sifa gani ya kuwa kiongozi, yaani amefika mahali sasa anaanza ubaguzi wa Watanzania Bara na Visiwani, anaanza kubagua jinsia, huyu hafai na lazima achukuliwe hatua.

“Namtaka anyamaze, asiendelee na mambo yake kwa sababu kama ataendelea kupiga porojo, nitasema mengi zaidi yanayomhusu kwa sababu siyo msafi kama anavyotaka kuwadanganya Watanzania,” alisema.

Habari kwa hisani ya Mtanzania Jumapili.

Mwenye nyadhifa Zake alizowahi kuzishika atuwekee hapa bayana tuone alivyozitumikia Kwa ufanisi
 
Naishauri chadema....kitendo cha sitta kufanya anayoyafanya ni mbinu hatari kwa chadema. Sitta atafukuzwa ccm, atahamia chadema na huo ndio mwanzo wa kufa kwa chadema. Huu ni mpango ulioandaliwa makusudi,sio bahati mbaya...subiri na uone then CHADEMA jaribuni kumpokea Sitta na mwone atakavokuja kuwavuruga kipindi cha uchaguzi...DONT TRY IT...DONT TRY PLEASE! Hawa mashetani watawamaliza mkifanya hivo...

Du.

Prince Tumbo

Huu ushauri au vitisho?!
 
Hahahaaaa...mtajiju.
Haya2husu!
Mafahali hao,ole wenu nyasi mlopo ndan ya kjan na njano.
 
Ni hatua muhimu kabla chama chochote hakijafa rasmi, je tumlaume Sitta au Mjenga kwa kutuonesha hatua chama kiliopo kabla ya kufa, ni sawa na kumlaumu yuda kwa kumsaliti yesu huku unashangilia kumwagika kwa damu ya yesu eti wewe umekombolewa.
 
Naishauri chadema....kitendo cha sitta kufanya anayoyafanya ni mbinu hatari kwa chadema. Sitta atafukuzwa ccm, atahamia chadema na huo ndio mwanzo wa kufa kwa chadema. Huu ni mpango ulioandaliwa makusudi,sio bahati mbaya...subiri na uone then CHADEMA jaribuni kumpokea Sitta na mwone atakavokuja kuwavuruga kipindi cha uchaguzi...DONT TRY IT...DONT TRY PLEASE! Hawa mashetani watawamaliza mkifanya hivo...

Du! Once beaten, twice shy. Huyu Sitta tayari alishawaangusha CDM ndiyo maana wanaumbuana kwenye majukwaa sasa. Lakini naona kama mwenye tatizo kubwa ni Sitta ambaye ni msahaulifu. Kamdanganya Mpendazoe naye kaingizwa mjini kwenye uspika. Sasa anahaha na sidhani kama atapata wa kumwokoa tena. Aibu kubwa zaidi ni pale wale wote aliowataja kuwa wako kambi moja wengine wakiwa mawaziri wenzake kumruka. Hivi itakuwaje watakapokutana kwenye kebineti? Viwango na speed naona sasa vimeanza kurudi kinyumenyume kwa kasi ya ajabu. Kama Sitta angetulia akaachana na siasa angeheshimika. Lakini kama hatabadilika huko tuendako ataaibika sana. Wabeja sana!
 
Back
Top Bottom