Khamis Mgeja aipa tano CCM

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1592933699563.png

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja amekipongeza chama hicho kwa kuweka utaratibu mpya wa kupata wagombea ndani ya chama.

Amesema kuwa utaratibu huo unajenga afya ya chama na kufufua matumaini kwa baadhi ya wanachama wagombea walio na sifa lakini siku za nyuma walikata tamaa kutokana na mazingira yake kuwepo mwenye nacho alitumia uwezo wake kupata uongozi hata kama hana sifa ya uongozi lakini ililazimu ashinde tu.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini, bw. Khamis Mgeja aliyasema hayo hivi karibuni alipotembelewa na waandishi wa Habari shambani kwake katika kijiji cha Nyanhembe Kata ya Kilago wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa lengo la kujionea shughuli za kilimo na ufugaji anazofanya hivi sasa baada ya kupumzika siasa.

Kada huyo wa chama cha Mapinduzi alisema kuwa uimara wa vyama vyovyote Duniani vilivyo bora na imara hujitathimini vyenyewe na kufanya mabadiliko ndani ya chama na kupelekea kujijenga zaidi na chama cha Mapinduzi CCM kikiwa kimoja wapo Duniani.
 
Kukaa kwako chini hakukupunguzii urefu au ufupi wa kimo chako.

Siasa ni kama tunda tu yapo mabichi, yalioiva, yakuoza na yasiyokomaa vizuri.

Karibu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom