Mwandishi wa Habari Khalifa Said amesema kuwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imekuwa ikitumia mamlaka yake kinyume na sheria kwa kuwachukulia hatua waandishi wa habari wanapotoa maoni yao, hasa wanapokosoa upande wa Serikali. Amesema kuwa jukumu la JAB ni kusimamia maadili ya uandishi wa habari, si kudhibiti maoni ya waandishi.
Katika video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook, Khalifa amesema kuwa waandishi wa habari wana haki ya kikatiba ya kutoa maoni yao kama walivyo watu wengine.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.