Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,643
- 31,594
SIKU MOJA NA KHALID ABEID MCHEZAJI WA SUNDERLAND, SIMBA NA TIMU YA TAIFA
Huwezi kuchoka kumsikiliza Khalid Abeid mchezaji wa Sunderland mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa 1970 baada ya Sunderland kuwa Simba.
Mimi na Khalid Abeid tuna ndoto ya muda mrefu ya kuandika kitabu chake katika maisha yake ya mpira kuanzia kwao Mwanza hadi anakuja Dar es Salaam kujiunga na Wekundu wa Msimbazi kisha kuondoka na kwenda kucheza mpira Arabuni katikati ya miaka ya 1970.
Maktaba ya Khalid Abeid imesheheni kumbukumbu ambazo kama una moyo hafifu utajifuta machozi kila dakika achilia yala maneno ya Khalid Abeid ambayo anaangalia mpira wa leo ulioko Tanzania na anafananisha na enzi zao
Khalid anasema, ''Washabiki wa leo wanashangaa wakimuona Morisson anapanda juu ya mpira.
Sunday Manara alikuwa akifanya sana hii tena yeye akipiga na saluti akiwa juu ya mpira na kafanya haya tukiwa katika timu ''combine,'' na tumeshashinda.''
Khalid Abeid ananikumbusha anasema, ''Yanga waliweka heshima Ghana kulikokuwa na timu za kutisha Afrika.
Yanga imekwenda sare na Asante Kotoko, kwao, Dar es Salaam na Addis Ababa
Ghana ilikuwa inaiheshimu Yanga.
Simba tumewafunga Hearts of Oak kwao timu kali kabisa Afrika katika wakati wao.''
Mimi na Khalid Abeid tumekaa tunasikitika kuwa hatuna Football Museum na sote tuna hofu kuwa historia ya mpira wa Tanzania itapotea.
Ukiangalia Maktaba ya Mpira ya Khalid unaweza kumwaga machozi.
Utamuona Shida Stua "full back," mstaarabu mwenye, "ball control," ya mchezaji wa mstari wa mbele.
Shida katangulia mbele ya haki.
Utamuona Abbas "Sungura" Dilunga "winger" mwenye kasi kubwa.
Abbas na yeye ametangulia.
Kuna picha ya Khalid na Nahodha wa Sunderland kaka yangu Yusuf Salum Maleta yeye na wenzake kama Arthur Mambeta walitokea Kahe Republic timu za mitaani zilikzokuwa na mpira wa viwango.
Nikiitazama picha hii Khalid mtoto mdogo nadhani haja fika hata miaka 20.
Khalid kanionyesha mkusanyiko wa picha za Timu ya Taifa akina Gulam, Nassor Mashoto, Salhina, Omar Zimbwe, Mohamed Chuma Omar Mahadhi.
Raha ya hizi picha ni pale ninapofananisha umri aliokuwanao Khalid na wachezaji wengine ambao walikuwa wamempita umri kwa mbali sana.
Khalid Abeid amenifungulia hazina yake ya picha ambazo zilitakiwa ziwe katika Museum ya Mpira kwa kuhifadhiwa kwa ajili ya kizazi kijacho.
Ukweli ni kuwa siku moja ni ndogo sana kwa yeyote yule kupitia Maktaba ya Mpira ya Khalid Abeid.