Njaa Mbaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 666
- 178
Ndugu wana bodi nimepitia utafiti wa twaweza na nimefanya survey kupata maoni ya wananchi wa kawaida sana juu ya nani anaweza kuibeba bendera ya CCM kuelekea ikulu 2015 nimeona wana mtu mmoja wa uhakika ni Wasira.
Edo kwa sasa ni ngumu mno kumuuza ukizingatia kidonda cha juzi cha escrow kimetibua kabisa na ya richmond.
Hivyo wananchi wengi wametibiliwa upya kabisa na ufisadi wa escrow na wameuunganisha na ule wa richmond ambao muhusika mkuu ni Edo.
Mkuu Kayanza nae alikuwa ameonekana kama angeweza kuibeba bendera lakini amepoteza matumaini kwa umma baada ya wananchi kuona hajui hata hela ya escrow ni ya nani. Hivyo ni heshima tu imembakiza kwenye UPM lakini wananchi hawana tena matumaini nae.
Mzee Sita yeye alijimaliza kwenye bunge la katiba hakuna tena mtanzania anafikilia tena hata yeye ameliona hilo.Mheshimiwa Membe ni mtu ambae kwa kweli amekosa kabisa mvuto na wananchi wengi hawampi kabisa nafasi ndani na nje ya CCM hivyo nafasi yake ya kubeba bendera ya chama kunako 2015 ni finyu mno.
Mwigulu ana hoja za wananchi maskini wa Tanzania ila watanzania wengi wanaona muda wake bado atakuwa kama JK 1995 dhidi ya Mzee Mkapa. J Makamba wengi wanamuona kama ni mtu mwenye ndoto ya uraisi lakinu watanzania wanamuona kama asiye na nafasi kwa aina ya rais anayehitajika kwa sasa.
Ngeleja na Pro. Tibaijuka wote tunajua wamechafuka hivyo siyo hitaji tena la watanzania. Sasa mtu ambae anaweza kubeba ajenda za chama na watanzania kwa ujumla ni comrade Wasira, ni mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja, mwenye kuijua historia ya nchi na mahitaji ya wananchi kwa wakati huu, asiye na makundi wala mitandao na mwenye kukubalika ndani na nje ya chama.
Haya ni baadhi ya mengi niliyoweza kuyatafiti juu ya hawa ambao wameonyesha nia ukizingatia kuwa bado CCM ina nafasi kubwa ya kushinda na kuongoza dola 2015. Ni nafasi sasa ya kuwafuatilia hawa waonyesha nia ili kuwajua kwa undani ndipo mtakubali mtu asiye na kashfa ya ufisadi ni Wasira na ndiye kete pekee ya CCM 2015.