Kesi za ukatili zakithiri Lindi

Kesi za ukatili zakithiri Lindi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Kati ya mashauri 652 waliyopokea wasaidizi wa kisheria mkoani Lindi, asilimia 80 ni ya ukatili, mgawanyo wa mali ya wanandoa wanapoachana na mirathi.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali Liwopac mkoani Lindi Cosma Bulu alisema hayo juzi wakati akizungumza na wadau wa sheria, wasaidizi wa kisheria na viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali wa mikoa ya Lindi na Mtwara

Alisema mashauri hayo yalipokewa na wasaidizi wa kisheria, wanaosimamiwa na shirika hilo.

Alisema kwamba madai ya ardhi, mgawanyo wa mali hasa wanandoa wanapoachana, ni mashauri yanyojitokeza kila mara.

Bulu alisema kwenye vijiji vingi kuna mashauri mengi kuhusu mgawanyo wa mali ya wanandoa wanapoachana. Alisema hadi Juni mwaka huu kuna mashauri 368 yakiwemo ya ukatili dhidi ya wanawake, mgawanyo wa mali na kesi za ardhi.

Wasaidizi wa kisheria waliopo kwenye ngazi ya kata na vijiji kwa kushirikiana na shirika hilo, huwasaidia wananchi kutatua kero hizo na zinazoshindikana hupelekwa katika vyombo vya kisheria.

Mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga alisema wasaidizi wa kisheria wako chini ya Liwopac na kuna wakati muda wao utaisha.

Hivyo, alisema halmashauri za wilaya na Manispaa, ziwatambue na kuwajengea utaratibu ili watatue kero katika jamii.

Ndemanga alisema kiwango cha mashauri kimekuwa kikipungua, kwa kuwa yanatatuliwa kwa wakati, badala ya kulundika kesi mahakamani.

Alilipongeza shirika hilo kwa kufanya kazi nzuri ya kusaidia kutatua kero za jamii ngazi za vijiji na kata.

1598870564306.png

1598870623781.png

Chanzo: HabariLeo
 
binadamu tuna siri nyingi sana.
ukute kawahiwa tu yeye ndo alianza uchokozi
vyovyote vile pole zake
 
Back
Top Bottom