Kesi yavuta makada wa ccm

Kesi yavuta makada wa ccm

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,680
Reaction score
37,867
na Grace Macha, Moshi




MAKADA mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mwenyekiti wao wilayani hapa, Godfrey Mwangamilo, jana walifurika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wakati kada wa chama hicho, Ramadhani Mwidadi maarufu kama ‘Gadafi’, alipofikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi. Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Ruth Mkisi, Mwanasheria wa Serikali, Twide Mangula, alidai kuwa Gadafi na wenzake sita walitenda kosa hilo Januari 21 mwaka huu.

Mbali ya Gadafi, washitakiwa wengine ni Mwenyekiti wa Kata ya Pasua, Abdulkadri Abdalah, maarufu kama ‘Tesha’ ambao wanatetewa na wakili, Godwin Sandi.

Mangula alidai, siku ya tukio washitakiwa kwa pamoja walikutwa katika Mtaa wa Benbela kwenye Manispaa ya Moshi na mabunda sita ya misokoto ya bangi.

Washitakiwa walikana shitaka na wako nje kwa dhamana hadi Februari 16, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Washitakiwa wengine ni Shabani Athumani Hasani, Ibrahim Islam, maarufu kama Masawe, Vincent Malasi, Hamisi Mtengeti na Amani Ngido.
 
Back
Top Bottom