PostGE2025 Kesi ya watuhumiwa 11 wa maandamano ya uchaguzi yaahirishwa, upelelezi bado haujakamilika

PostGE2025 Kesi ya watuhumiwa 11 wa maandamano ya uchaguzi yaahirishwa, upelelezi bado haujakamilika

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Kesi inayowakabili watuhumiwa 11 kati ya 172 wanaodaiwa kuhusika na matukio ya uhalifu yaliyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imeahirishwa hadi Novemba 26 mwaka huu baada ya upande wa mashitaka kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Watuhumiwa hao upande wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza wamekuwa wakipandishwa mahakamani kwa awamu, wakikabiliwa na mashitaka mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali ya umma, unyang’anyi wa kutumia silaha na kufanya maandamano bila kibali.

Shauri hilo limetajwa leo Novemba 17, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ramla Shihagilo, ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Mahembega Elias, alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi bado haujakamilika na kuomba kuahirishwa shauri hilo.Kesi imeahirishwa hadi Novemba 26.
 
Akili ya mama hiyo, kesi kupigwa dana dana muda uende...kama ulivyokuwa kesi ya Lissu pale kisutu!.
 
Mahakama zimeshindwa KUSIMAMIA haki ni zamu ya mahakama KUU zaidi kutenda haki
 
Back
Top Bottom